Header Ads

test

Najuta Kumsomesha

 

NAJUTA KUMSOMESHA
Najuta leo najuta
Majuto ni mjukuu
Mwenzenu yamenikuta
Nimeshavunjika guu
Wakubwa walinambia
Masikio nikaziba.
Hata ada nikalipa
Chuoni kumpeleka
Nikajiona kibopa
Kidume nimeshafika
Kumbe aniangalia
Atimize zake ndoto.
Leo chuo kahitimu
Hataki kunisikia
Kweli mi mwendawazimu
Tayari nimeumia
Mi mjanja wa mjini
Hadharani nimepigwa.
Bora bata ningekula
Kuliko nivyojinyima
Kweli mimi ni mbulula
Akilini si mzima
Kosa hili nilofanya
Daima nitajutia.
Nilijua akisoma
Maisha tutayajenga
Kidume nikajituma
Mihela kumtumia
Kumbe akiwa chuoni
Mwingine alimpata.
Leo kanitamkia
Mi siyo wa levo yake
Mrembo kanikimbia
Ameniacha mpweke
Najuta mimi najuta
Najuta kumsomesha.

Idd Ninga
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com

Hakuna maoni