Mama wa Thamani
MAMA WA THAMANI.
1)Dua njema nakombea
Mama ngu ulonilea
Mpaka Leo nimekua
Japo kwako ni mtoto.
2)Mengi nimeyapitia
Kipindi kile nakua
Leo mama natambua
Jinsi ulivyonilea.
3)Hakika uliumia
Machungu ukasikia
Ulipoona nalia
Hukusita bembeleza.
4)Cha kukulipa ni nini
Cha thamani duniani
Hata kama ni madini
Yawezi kutosheleza.
5)Namuomba Rahamani
Akupe sana imani
Muumba wetu manani
Akuzidishie kheri.
6)Izidi yako imani
Mama yangu wa thamani
Mfano e duniani
Hakuna wakutokea.
7)Moyo wapata amani
Furaha yatoka ndani
Najiona wa thamani
Nikonapo mama yangu.
8)Thamaniyo kubwa sana
Kwako mama najichana
Nywele uliponchana
Hakika nilipendeza.
SHAIRI-MAMA WA THAMANI.
MTUNZI-Idd Ninga,Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Post a Comment