NAKUPENDA SI UTANI
1)Mwenzako mi sina raha,sipokuona usoni
Inatoweka furaha,ninajawa na huzuni
Nahisi ninajeraha,niloumia moyoni
Yanitoweka karaha,yaja raha ya rohoni
Nakupenda si utani,najianda kukuposa.
Inatoweka furaha,ninajawa na huzuni
Nahisi ninajeraha,niloumia moyoni
Yanitoweka karaha,yaja raha ya rohoni
Nakupenda si utani,najianda kukuposa.
2)Najianda kukuposa,posa nilite nyumbani
Naapa sitokutosa,ukingia mwangu ndani
Nitaepuka mikasa,nomba hilo kwa manani
Kwako sitofanya kosa,niingie hatiani
Nakupenda si utani,kubali nitakuoa.
Naapa sitokutosa,ukingia mwangu ndani
Nitaepuka mikasa,nomba hilo kwa manani
Kwako sitofanya kosa,niingie hatiani
Nakupenda si utani,kubali nitakuoa.
3)kubali nitakuoa,ni wewe siyo Fulani
Yeye iwake natania,siyo kweli ni utani
Hata yeye anajua,wewe ndo upo moyoni
Tena ameniambia,nisikuache njiani
Nakupenda si utani,taka uwe mke wangu.
Yeye iwake natania,siyo kweli ni utani
Hata yeye anajua,wewe ndo upo moyoni
Tena ameniambia,nisikuache njiani
Nakupenda si utani,taka uwe mke wangu.
4)Taka uwe mke wangu,unifae maishani
Uwe ni furaha yangu,hata kama ni gizani
Niwatambie wenzangu,nimshukuru Rahmani
Kunipa chaguo langu,nililowaza zamani
Nakupenda si utani,wambiue wazazi wako.
Uwe ni furaha yangu,hata kama ni gizani
Niwatambie wenzangu,nimshukuru Rahmani
Kunipa chaguo langu,nililowaza zamani
Nakupenda si utani,wambiue wazazi wako.
5)Wambie wazazi wako,posa niilete lini
Waleze na ndugu zako,ndoa iwe siku gani
Sema kwa mdomo wako,mahari yo iwe nini
Sijiwezi mi mwenzako,tena nipo taabani
Nakupenda si utani,siwezi penda kwingine.
Waleze na ndugu zako,ndoa iwe siku gani
Sema kwa mdomo wako,mahari yo iwe nini
Sijiwezi mi mwenzako,tena nipo taabani
Nakupenda si utani,siwezi penda kwingine.
6)Siwezi penda kwingine,kule mi sipaamini
Sitokuacha pengine,nitoweke duniani
SItowapenda wenghine naogopa mitiohani
Ujue jambo jingine,taka fanya nusu dini
Nakupenda si utani,natungo nakutungia.
Sitokuacha pengine,nitoweke duniani
SItowapenda wenghine naogopa mitiohani
Ujue jambo jingine,taka fanya nusu dini
Nakupenda si utani,natungo nakutungia.
7)Natungo nakutungia,kalamu ipo mezani
Ndugu nimewaambia ,wote wa kwangu nyumbani
Mama amefurahia,sema takuona lini
Nambie nitamwambia,utakuja siku gani
Nakupenda si utani,nambie nipoe moyo.
Ndugu nimewaambia ,wote wa kwangu nyumbani
Mama amefurahia,sema takuona lini
Nambie nitamwambia,utakuja siku gani
Nakupenda si utani,nambie nipoe moyo.
SHAIRI –NAKUPENDA SI UTANI
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160.
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160.
Post a Comment