Header Ads

test

Mchumba Hasomeshwi

 






Kakudanganya nani,
Unipeleke chuoni,
Hukumuona Hassani,
Livyokufa kitanzini,
Kisa kuzama penzini,
Na kumsimesha Jasmini,
Ulijizima fahamu Eee!!!
Mashairi unaghani,
Na kurusha mtandaoni,
Acha ulumbukeni,
Hizo swaga za kizamani,
Nenda mahakamani,
Ada uidai kizimbani,
Una jeuri hiyo???
Kutenda kosa si kosa,
Bali kurudia kosa,
Usingepuuza walokuasa,
Nyumbani ungeleta posa,
Na kunioa kabisa,
Padri akatutakasa,
Labda nisingekutosa.
Mshahara wa dhambi ni mauti!!!
Nilikupenda kwa dhati,
Nikakuona wa thamani,
Kwako nikajizatiti,
Sikujua ya mbeleni,
You know what?
Nilipohitimu nikabaini,
Nilikua punguani,
Kupenda level za chini,
Mchumba hasomeshwi Babu!!!
Akili imepambazuka,
Fahamu zimepanuka,
Nimepata aloelimika,
Mbali nae nitafika,
Kuwa nawe muuza duka,
Wenzangu watanicheka,
Pole Idd Ninga , hudumia wateja.
0752371890

Hakuna maoni