Ushairi katika zama za utandawazi.
Huseyn Jafari Juma
USHAIRI NA MSHAIRI KATIKA ZAMA ZA UTANDAWAZI
Tar 21/ 3 kila mwaka ni siku ya ushairi duniani. siku hii imeanzishwa na shirika la umoja wa mataifa linakoshughulika na elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO) mwaka 1999 kwa lengo la kuhamasisha usomaji, uchapishaji, ufundishaji wa ushairi duniani kote
Marekani na Kanada wameichagua tar 15/10 kama siku Ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mshairi mkongwe wa kiroma Publius Vergilius Maro aliyezaliwa 15/10/70BC
Lakini siku hii ya ushairi kwa nchi kama uingereza husherehekewa alhamis ya kwanza ya mwezi wa 10 kila mwaka ambapo mwaka huu itakuwa tar 4
Kwahiyo Uingereza, marekani, na kanada wamechagua mwezi wa kumi katika kusherehekea siku ya ushairi duniani
HISTORIA FUPI YA USHAIRI
Wataalamu wengi wa fasihi wamekubaliana kuwa ushairi ulianza kipindi ambacho binadamu alianza kutumia lugha
Kwa maana kuwa wanahistoria wanaamini kuwa binadamu alipitia hatua mbalimbali za ukuaji
Kuanzia mnyama mwenye kutumia miguu minne
Mnyama anayetumia miguu Miwili
Mpaka kwenye hatua ya kutoka kwenye unyama na kuwa mwanadamu kamili na katika hatua zote hizi a mwanadamu ilikuwa ni mbinu za kukabiliana na mazingira yake
Baada ya kuwa binadamu kamili ndipo alipovumba lugha na hapo ndio ikawa chanzo cha ushairi
Hapo awali ushairi ulitumika katika shughuli mbali mbali za kijamii kama matambiko na shughuli za uzalishaji mali kama kilimo, uvuvi, n.k
Katika shughuli za kiuchumi Mashairi yalitumika kuhamasisha... Tamaduni hizi zipo hadi leo kwa mfano kwenye jamii za wadigo na wasukuma
Kabla ya mwanadamu kupata maendeleo ya kisayansi na kitknolojia ushairi ulihifadhiwa kichwani pekee na hiyo ndio ilikuwa njia ya kurithisha ushairi kutoka kizazi kimoja kwenda Kingine
UMUHIMU WA USHAIRI DUNIANI
Kwa miaka yote ushairi umekuwa muhimu zaidi katika jamii zetu
1) ushairi umekuza na kuendeleza lugha nyingi duniani ikiwemo kiswahili
Kwa miaka mingi washairi wamekuwa na kazi kubwa ya kukuza na kuendeleza lugha kupitia kazi zao
Mbinu za kutunga maneno mapya, kazi zao mufti zimeweza kueneza lugha na kukuza lugha
Lugha ya kichina, kigiriki, kilatini, kiarabu na kiswahili ni miongoni mwa mifano bora
2) Ushairi umeleta usawa na kuzikomboa jamii nyingi duniani
Nchi nyingi zilizotawaliwa, zilitumia ushairi kama njia ya kueleza mawazo yao juu ya watawala, na pia kuhamasisha watu kujua haki na wajibu wao
Pia ushairi umehamasisha watu kupigania uhuru kwa nchi zao
Kwa mfano Tanzania walitumia mashairi ya kiswahili kufanya hivyo
Lakini pia ushairi ulitumika kwenye harakati za mtu mweusi huko marekani
3) Ushairi unaibua matatizo yanayoikumba jamii na kuyatolea suluhisho
Ushairi umekuwa ukiibua matatizo mbali mbali ya kijamii na kuyatolea masuluhisho.. Mfano uongozi mbaya, maisha magumu, mmomonyoko maadili n. k
4) ushairi ni burudani
moja wapo ya lengo kuu la ushairi ni kuiburudisha jamii ...maaana hata asili yake ni kumtoa binadamu katika upweke na uchovu ndiko kulikoleta ushairi
Zama zilizopita ushairi ulikuwa ndio burudani nzuri zaidi
Wafalme wengi walikuwa na washairi wao wa kuwaburudisha
Pia mtume Muhammad ('s. a. w) alikuwa akipenda mashairi na alikuwepo mtu wa kumghania mashairi
USHAIRI NA MSHAIRI
Tumeona historia fupi ya ushairi, tumeona umuhimu wa ushairi katika jamii lakini Katika sehemu hii tutaangazia namna gani ushairi unavyomfaidisha mshairi
Tumeona wacheza mpira wakipata pesa nyingi kutokana na mpira na fani nyengine kadhalika
Je mshairi anafaidika na ushairi wake??
Hili ndio swali kuu na ndio msingi wa mada hii
Kama nilivyosema hapo awali kuwa zamani washairi walikuwa wakiwaburudisha wafalme, lakini pia washairi walikuwa wakighani mbele ya watu wakapata kitu cha kuendeleza familia zao. Kwa mfano mshairi wa zamani aliyejulikana kama Raphael na shairi lake la The Parnassus
Baada ya maendeleo ya sayansi na teknolojia maandishi yaligunduliwa na hapo ndipo ushairi ukaingia katika hatua nyengine ya uhifadhi
Mashairi yakaanza kuandikwa kwenye vitabu
Maendeleo haya yalimpa mwanya mwengine Mshairi aweze kukusanya mashairi yake na kuandaa kitabu ambacho aliwauzia watu na faida yake hutegemea na nakala alizouza
Na pia faida hutegemea jamii iliyomzunguka mshairi kama ni ya wanaopenda kusoma vitabu basi atafaidika kama sio hivyo basi hakuna apatalo mwandishi kwa mfano mtu kama Aristotle aliandika vitabu vya ushairi na pia kuzungumzia ushairi kwenye kitabu chake cha Poetics
Mshairi wa kichina pia alindika The Shijing
Kukosekana kwa faida katika fani hii imepoteza washairi wengi walio na vipaji ni washairi wachache saana walioweza kujitosa katika fani bila kujali faida
Lakini leo napenda kumzungumzia mshairi wa kiswahili katika zama hizi za teknolojia
Tukumbuke kabla ya hati hizi za kiswahili tunazozitumia Leo hii, kiswahili kilikuwa kikitumia hati ya kiarabu
Na baadae ndipo waingereza walibadili hizi hati tunazotumia leo hii
Na pia tukumbuke ushairi wa kiswahili umepitia mikono ya washairi maarufu kama Mwengo Bin Athuman 1728-1840 aliyetunga utenzi wa kwanza wa kiswahili UTENZI WA TAMBUKA, Muyaka Bin muyaka, Shaban Robert, n.k
Lakini hawa wote walikuwepo kipindi cha maandishi tu hivyo wakawa wamejikita katika kutoa vitabu pekee
Maendeleo ya sayansi na teknolojia huiamisha jamii kutoka katika aina flani ya maisha kwenda aina mpya ya maisha
Ni hivyo hivyo kwenye ushairi kuwa baada ya kugunduliwa kwa maandishi washairi walianza kuaandaa vitabu na kuyahifadhi mashairi yao kwenye maandishi
Tokea kipindi hiko uuzaji wa vitabu ndio ilikuwa njia kuu ya ya kumpatia kipato mshairi
Hadi leo hii bado uchapishaji wa vitabu ndio njia kuu ya kumpatia kipato mshairi
Hali inayoleta changamoto kwa washairi wengi hasa ukizingatia jamii za waswahili si zenye kupenda kusoma vitabu
Lakini Changamoto kuu walizonazo washairi wa kiswahili ni mbili
1) kutokuwa wa bunifu
Kitu chochote kinachokosa ubunifu huisha ladha mbele ya jamii kwahiyo ushairi wa kiswahili umekosa ladha mbele ya jamii hasa kutokana na washairi wenyewe kukosa ubunifu juu ya fani yao
Ni ubunifu gani ninao uzungumzia hapa
Kwanza lugha , lugha ndio jambo muhimu katika ushairi.. Ushairi ni sanaa inayotumia lugha ya mkato katika kuwasilisha mawazo ya mshairi mwenyewe sasa ikiwa washairi wanakosa ubunifu katika lugha zao inakuwa ngumu kuivutia hadhira husika ili waweze kuipenda kazi yako
a) uteuzi wa maneno
b) uwasilishaji wa mada
c) uchaguzi wa mada
d) lugha ya picha na mbinu nyengine za kisanaa
Kama mshairi utafanikiwa katika vipengele hivyo vinne basi bila shaka mashairi yako yatakubaliwa na jamii
Na hatimae kuanza kufaidika na matunda ya ushairi
2) washairi kuwa mbali na teknolojia
Kuchapisha vitabu ni jambo muhimu lakini kama wanataka kufaidika na ushairi wao ni lazima waendane na kasi ya teknolojia iliyopo
Kwa mfano kwa sasa watu wengi wamehama katika kusoma vitabu vya hard copy bali wanaenda kusoma online
Watu wengi wapo instagram na YouTube
Hivyo inatakiwa washairi wawafuate huko huko kwa ubunifu wa kazi zao
Kwa mfano waanze kughani mashairi yao kisha waya weke kwenye YouTube kazi zikiwa nzuri ni lazima watu watayaangalia tu hivyo wanaweza kupata malipo kupitia YouTube na pia kujitangaza mbele ya jamii
Kuandaa Video fupi za mashairi na kuzipeleka instagram hii pia itasaidia kuwatangaza washairi na kupata wafuasi wengi wa kazi zao
Hivyo vitu viwili kama vitafanywa kwa ubunifu wa hali ya juu unaweza kumsaidia mshairi kwa kiasi kikubwa
Kupitia kazi hizo unaweza ukapata matangazo ya bidhaa kupitia Kazi yako
Pia kama shairi lako ni zuri linaweza kuwa ni muito kwenye simu za watu kwani ukumbuke si watu wote wanapenda kutumia nyimbo kama miito kwenye simu zao hivyo washairi wanapoweza kutunga kazi zao nzuri zinazoendana na wakati kuna uwezekano Mkubwa wa kufanikiwa
Tunga mashairi yanayoendana na wakati
Ya kiislamu, kikristo, ya kimapenzi, ya kuchekesha, kuhusia, mapenzi ya mama, mapenzi ya mke kwa mume, na mume kwa mke, mashairi yanayoendana na wakati au yaliyotawala vichwa vya habari mitandaoni
Yote hayo yanaweza kukusaidia katika kukutangaza na kukupa faida hata baadae utakapo toa kitabu kinaweza kupata soko
JE HAYO YATAWEZEKANAJE
kuna mambo yanawezwa kufanywa na Mshairi peke yake kama kuanzisha chanel ya YouTube, kuangazia instagram
Lakini kwenye masuala ya kampuni ni lazima vyama vya ushairi viwe imara na kuanzisha makongamano na kuwashirikisha makampuni makubwa kama makampuni ya mitandao, vinywaji, n.k na kuwaelezea ni kwa namna gani mnaweza kushirikiana nao katika kutangaza biashara zao kupitia fani za ushairi ila kabla ya kuanzisha hayo makongamano wanatakiwa washairi wenyewe watie bidii katika kujitangaza kwa kazi zao ziwe nzuri zaidi
Lakini pia kuna swala la kupeana nafasi kwamba sio kila mshairi anaweza kughani na sio kila mghani anaweza kutunga hivyo mshairi asieweza kughipatet anatakiwa atoe nafasi kwa mtu Mahiri wa kughani ili Kazi yao ipat ubora unaostahiki
TUKIFANIKIWA JUU YA HILO TUNAWEZA KUPATA FAIDA YA USHAIRI.
tutakuwa tumeifikia jamii kwa kiasi kikubwa
Na pia itakuwa tunaongeza kipato kupitia ushairi
Ahsanteni
NB: naruhusu kukosolewa na maoni kwa hichi nilichokiandiaka
Andiko hili limeandaliwa na Mwl. Hussein Jafary Juma
(kipanga mtoa)
0713115683
Tar 21/3/2018
Mwanza - Tanzania
Post a Comment