Nadharia ya Ushairi
Makala hii imeandikwa na Hamisi Kisamvu,Dar es Salaam,2018
Awali tuangalie mapito ya mangwiji wa fani hii jinsi walivyoelezeaa "utungo ufaao
yoyote ni kiumbe kiishicho miongoni mwa watumizi wake, nimetamka kiumbe, lakini sisemi
eidha ni chenye uhai ama sicho hiyo ni nafasi yako wewe unayenisoma kutoa maamuzi
ya tamko stahiki baada ya kunielewa vyema.
Katika sifa ya kiumbe lugha ni pamoja na kuzaliwa, kula, kukua, na pia kufa. Kama
vilivyo viumbe vingine mbalimbali vilivyopo ulimwenguni, tofauti iliyopo kati ya viumbe
vingine na kiumbe lugha ni kwamba sifa ya kiumbe lugha hutegemea sana majaaliwa ya
watumizi wake. Hii inashabihika kwa kuwa waneni wa lugha husika ndio wavunjikao
mabega kwa upagazi wa majukumu kuanzia awali, nako ni kuizaa lugha yenyewe yani
kuifanya iwepo (kuiunda) na kuendeleza ulezi wake kwa kuilisha yani; kuiongeza
misamiati inayopatikana katika lugha hiyo au hata nje ya lugha hiyo kwa kuzingatia
vigezo vinavyokubalika, lakin pia jukumu lingine ni kuikuza lugha na hapo ndipo
kunapatikana matendo kama ya kuiboresha lugha, kuifundisha lugha na kuieneza. Na bila
ya kutenga sifa ya nne kwa kuiona tu yamkini ni mbaya! La hasha, hiyo ipo na inaweza
kutokea nayo ni kufa kwa lugha. Na
kama nilivyo tanabahisha hapo nyuma kifo chake
kinaweza kutokea kwa kubarikiwa na
viumbe wanaoizungumza lugha hiyo.
Uharamia usiofaa kuvumilika ndio
hasa Baraka yenyewe iwapo wadau wa lugha hiyo
watauvumilia nakuacha uendelee
kufanyika katika jamii hiyo, na si mwingine isipokuwa
ni kuipotezea “kiumbe lugha” sifa
zake mbili katika hizi nne nilizotaja awali nazo ni
kuilisha na kuikuza lugha, hizo
ndizo sifa ambazo zinaweza kuifanya lugha ipate nguvu
na kuenea hata katika jamii nyingine
nako ikazungumzwa, ikapendwa na ikazoeleka. Na
haya mawili yasipofanyika kwa
uchungu wa kimalezi kama wa mzazi na mwana ni
dhahiri kwamba lugha hiyo inaweza
kupotea na huko kukawa ndiko kufariki kwake. Ni
msiba mzito utukapo ndani ya jamii
husika.
Chimbuko la lugha iitwayo
”kiswahili” kwa kiasi kikubwa ni kichangizi cha maneno
yatokanayo na lugha za asili za
wakazi wa mwambao wa pwani ya Afrika Mashariki,
ingawa kwa tamko hilo haimaanishi
kuwa hakuna ziada ya misamiati iliyoingia
ndanimwe toka katika zile zisizo za
asili, hapana! Kiswahili kina athari kubwa sana
inayotokana na maneno ya wageni
waliotujia katika upande huu wa eneo la dunia
kuanzia karne nyingi zilizopita.
Tafiti zinaonesha kuwa kiarabu
ndicho kinachoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya
maneno katika hazina ya misamiati ya
lugha ya Kiswahili ikifuatiwa na kiingereza na
kireno nk.
Pia kuna usemi usemao kwamba
Kiswahili ni kibantu, napata picha kuwa ina maana
wabantu ndio wamiliki halali wa
lugha hii adhimu ya “wasahel” (tamko la waarabu
likiwa na maana ya watu wa pwani )
waswahili.
Kwa mtiririko wa mtazamo ulio
dhahiri nadiriki kukosa kigugumizi cha kusema kuwa
kinadharia Kiswahili ni lugha ambayo
uwepo wake ulianza pale ulipo patikana uwepo
wa wakazi katika ukanda wote ambamo
lugha hiyo inazungumzwa yaani; Kiswahili ni
lugha ambayo ilikuwepo kabla ya
kuwepo.
Na kwa kwa hali hiyo haina shaka
kuwa fasihi ya lugha hii nayo pia ilikuwapo kwa
ukamilifu wake ikiwa ina kusanya
fani na tanzu zake, ingawaje kulikuwepo na tamaduni
zilizohitilafina miongoni mwa
makabila hayo ya mwambao mwa pwani. Hapa napenda
kuusemea zaidi “utanzu” wa ushairi
katika fasihi nzima, utanzu ambao kama ilivyo lugha
yenyewe wafatilizi wengi
wametofautiana katiaka kuelezea muda ama kipindi ambacho
utanzu huu ulianza kuwapo katika
Kiswahili.
Katika kipindi fulani nyuma
iliaminika kuwa ushairi wa Kiswahili ulinzia kaskazini mwa
pwani ya Kenya kunako karne ya kumi
masihiya(M) au kabla, kisha ushairi huo ulienea
kuelekea kusini na kufika mrima
(pwani ya Tanzania) na Zanzibar kwenye karne ya kumi
na tisa mawazo hayo yalitolewa na
wataalamu wa mwanzo wa historia ya ushairi wa
(1988). Hata hivyo marehemu Chiraeghdin yeye alitoa kauli inayoonesha uoni wa mbele
zaidi ya wenzake na kukiri kuwa huenda utafiti zaidi ukakanusha au kuthibitisha dai hilo.
“katika uchunguzi wa arudhi ya Kiswahili uliofikiwa mpaka sasa ni kuwa tarekhe ya
ushairi wa Kiswahili kama ilivyo lugha yenyewe ilianzia uswahilini yani sehemu za
kaskazini katika mwambao ambao lugha imeambaa. Hata kufikia mwisho wa karne ya
kumi na tisa utunzi wa ushairi ndipo ulipo jitokeza sehemu za mlima na visiwa
vilivyokabili. Yamkini kila utafiti ukizidi kufanywa huenda ikapatikana ithibati kuwa
hivyo sivyo......(1977:8)” huyo ni Chiraghdin.
Lakini pia kuna ukomelezi wa Mulokozi na Sengo (1995:3-5) wao walitoa nadharia tofauti
na kusema kuwa ni makosa kudai kuwa ushairi wa Kiswahili ulianzia katika eneo moja tu
na kisha kusambaa katika eneo lingine, kwani ushairi huambatana na lugha na utamaduni
na madhali hakuna jamii isiyo na lugha na utamaduni hakuna jamii isiyo na ushairi.
Hivyo ushairi wa Kiswahili haukuanzia mahala pamoja tu na kisha kusambaa kwingineko
bali ulichipuka katika maeneo yote ya uswahilini takriban wakati uleule walipochipuka
waswahili wa jamii inayohusika. Haiyumkiniki kuwa waswahili wa upwa wa kusini wa
mtang’ata, unguja, pemba, mzizima, kilwa, mafia, lindi na Mtwara walikuwa mabubu
wasioweza kutunga au kuimba mashairi hadi walipoletewa ushairi wa waswahili wa
kaskazini kwenye karne ya kumi na tisa!
Na hivyo ndivyo nionavyo mie
Post a Comment