Ushaha ni Nini ?
Mtunzi:
Mohamedi Bakari
Al Mufti
Mombasa,Kenya
Yuwauza muuzaji, ushaha ni kitu gani?
Aomba ujulishwaji, apate yake bayani,
Ili utatizikaji, uuke mwake kitwani,
Ushaha ni n'ni kwani?,
Haulizi mulizaji, ela hutaka undani,
Kujuzwa anataraji, ili atoke kizani,
Hubaki ni mngojaji, wa jawabu yenye shani,
Ili akae mwangani,
Muf'ti si mjibuji, wa jambo hili ugani,
Sina mwanga wa buruji, nielezeto maani,
Shaha haswa huwa nani?
Jambo lataka wambuji, waliovama kungani,
Apawae hili taji, la ushaha ulingoni,
Huwa ni mbobeaji, aliyekita tungoni,
Tungo zake ni siraji, zenye hikima pomoni,
Zikongazo mioyoni,
Ki nyaka ni mkongaji, hawi ni kijana sini,
Nguli wa utongoaji, maneno kwa umakini,
Hawi ni m'banangaji, wa lugha matamshini,
Mkwasi kiswahilini,
Nadhani msailiji, hajakinai katwani,
Nami kuvuka biriji, nimesaki twarikani,
Wait'ezao diriji, nimewapa usukani,
Watupe ukalimani,
Sijawami muambaji, hapa nefika kingoni,
Suala hili ni maji, yalonizidi kimoni,
Naita watasuwaji, hebu hukuno nd'ooni,
Mutoe yenu maoni,
Post a Comment