TAMTHILIA YA KULOGANA,Ushairi na hisia
TAMTHILIA YA KULOGANA
USHAIRI NA HISIA
Jukwaa linawaka taa,waigizaji wamejipanga jukwaani kila mtu sehemu yake,mtemi amekaa katika kigoda chake,mkoni ameshika bakora ndefu ilofungwa kwa manyoya ya mkia wa kondoo.
kyomopoet anaingia jukwaani akiyumbayumb ,mkononi kabeba chupa ya soda.
KYOMOPOET- Nyie hamniwezi hata kidogo,mimi ndio baba lao hapa kijijini
WATU-aaah,una nini wewe ?
KYOMOPOET-nani ananiita mimi mlevi wakati sijalewa,yani kunywa maji ya madafu ndo mnipigie kilele
WATU-ha !.huyu nae katokea wapi
KYOMOPOET-i am think you down.sit sir
WATU-sawa nidharauni ila hata mimi ni mjuzi kama nyie,ngoja niwapeni dawa yenu mkae chini.
HAUTOMUONA KWA KUMTAZAMA
Nilipomtazama nikampenda pasipo kumuangalia,
sababu nilimuona kwa kumtazama pasipo kumtazamia.
Sasa nimemuona, Baada ya kumuangalia.
Nimegundua alivyo
ni tofauti na nilivyomtazamia
, ndiyo maana sichoki
muangalia na macho kumkodorea.
Yaani kwa picha ukimtazama ni mzuri wa sura umbile mpaka nadharia,
ila ukimuangalia utagundua yupo tofauti na nilivyomtazamia
Ndiyo ni mrembo,Haonyeshi kama ni batili,
Sema ni msiri anayemjua dhahiri ni wake Jalali
Akizungumza huku ukimuangalia hautotazamia
kusikia anavyoweza kukuzungumzia.
Hapo ndipo nilipojifunza, Usimpende mamalia kwa namna alivyojinawiria
Usimpende mamalia kwa namna utakavyomuangalia
Usimpende mamalia kwa namna utavyomsikia,
Maana ataweza kukwambia yale utakayo yasikia ama kukufanyia upendayo kufanyiwa. Mpende mama
Lia kwa namna anavyokupenda pia, maana upendo hauna sababu rasmi .
Ila huwa rasmi upendo ukipata pendo na hapo ndipo penzi huchipua rasmi.
George Kyomushula
MTU MOJA-mtoeni huyu kaja kutuharibia kikao chetu,sisi tupo hapa kumtafuta nani mchawi yeye anatuimbia nyimbo zake za kizungu hapa,fukuza huyu.
(watu waili wanainuka na kwenda kumtoa Kyomopoet hadi nje ya jukwaa.)
MTEMI-Enhee hebu niambieni ni nani aliekwenda kumuwangia mwenzake katika kijiwe chake cha kuuzia samaki pale magogoni ?
MKANYA-mimi ni simba hakuna wa kuniweza katika kijiji hiki,nyie nyote watoto wadogo sana.
WATU-aahhhhh dharau hizo
MKWANYA-mnasema,kweli nyani haouni.........basi tu msije sema nawatusi ila sikilizeni
SIMBA
Kufa ndio kufariki, hasa afariki mwamba
Mwenye sifa na miliki, lofa hakosi kutamba
Nawe kama husadiki, waangalie manamba
Sababu simba ni simba hafi sawa samaki
SHETANI KATAJA JINA
Taireni wa viremba, wa hati na wa tunguli
Taireni nawaomba, mshike njia ya kweli
Msimchezeshe rumba, wala kumuweka mbali
Kutii amekubali, jina ametoa amba

Hafi sawa na samaki,sababu simba ni simba
Maiti haifichiki, ina sharubu na fumba
Mkia haukunjiki, na ufanane na kamba
Sababu simba ni simba hafi na sawa samaki
Hachomeki mishikaki, wanamjua walumba
Japo mshikwe na dhiki, muenda nani kuomba
Makundi na halaiki, nyamae ngumu kuramba
Sababu simba ni simba hafi sawa na samaki
Sokoni hanunuliki, japo mboga zikiwamba
Na kuuzwa hauziki, upate gonga usumba
Jipumzishe rafiki, hatoelewi kwa pumba
Sababu simba ni simba hafi sawa na samaki
Kama kiburi na chuki, ni tabia za wajomba
Walio shika mikuki, na kwenda kumperemba
Na simba hajafariki, kwanini kote kugomba?
Sababu simba ni simba hafi sawa na samaki
Watama mbali sifiki, yatosha nilo yaamba
Siku ya hiki na hiki, simba nivae kiremba
Na hapo si kamatiki, kila mwali kumremba
Sababu simba ni simba hafi sawa samaki
MKANYAJI
RANGI-Mtemi umeona sasa nilichokwambia,huyu jamaa mchokozi sana,yani yeye kanitisha kule kwenye kibanda changu na sasa anakuja kunitisha huku tena mbele yako,mkanye.
MKANYA-mi sijakosemea wewe.
RANGI-mtemi ni kweli kabisa hadi najuta kabisa kuwa nae mtaa mmoja,yani mtu anatusumbua watu usiku,hatulali kwa ajili yake,yani kaniweza kabisaaaa kaniweza
KANIWEZA!
Kaniweza kaniweza, huyo aliyeniroga,
Kutunga kwanitatiza, hata kichwa nikipiga,
Vina vyanipotea, mizani naivuruga.
Kaniweza!
1)Naona mnalumbana
Robo nusu kutukana
kwa magego mwaumana
mnataka kumezana
Ndita mwaangaliana
Sura mmekunjamana
kuna lipi la maana
Eti mnachezeana
mchezo wa kulogana
Mmeanza kutishana.
2)Kunani enyi mabwana
Kwanini kuna zozana
Uchawi kutupiana
Mnazidi daiana
Usiku mwachukuana
Angani mnapishana
Ubabe mwaonyeshana
Kwa vineno mwashindana
Sidhani mnajengana
Ndugu mnaboana.
3)Tungo mnapotezana
Ama mnataniana ?
Mlikwisha ambiana
Jifanye mwajitukana
Hilo twajichanganyana
Nona ndoto ya mchana
Ndugu wili kugombana
Wakti mlifundishana
Pale mlipokosana
Ni wajibu kupatana.
4)Kama toto mwafinyana
makonzi mwapigiana
Wote para mwanyoana
Na maji mshatiana
Ka duma mwakimbizana
Ohoo mnanyatiana
Bora mngelipatana
Na mikono kupeana
Atakavyo maulana
Ni haramu kugombana.
SHAIRI-ACHENI KUGOMBANA
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160

Kaniweza si katiti, wenzangu nawaambia,
Kutunga japo baiti, uzito waniingia,
Nimeshindwa kusukuti, leo nawapasulia,
Kaniweza!
Kaniweza mtotongwa, kutunga sasa siwezi,
Ni dhahiri nimekwangwa, kanipitia mlozi,
Na akili nimefungwa, kwa ndumbaze na hirizi,
Kaniweza!
Kaniweza kila jambo, ya utunzi wa nudhuma,
Kunichukia mwajimbo, athama huku kuvuma,
Alianza na vikumbo, sasa majini katuma,
Kaniweza!
Kaniweza tena khasa, kwa wino wangu kumwaga,
Lakini ajuwe sasa, mwili naenda ukaga,
Zatosha hizi khamsa, sina budi kuwaaga,
Kaniweza!
25 Desemba 2017 Jumatatu 08:33am
Jina la Mtunzi Dotto Rangimoto
Jina la Utunzi Jini Kinyonga
Simu +255762845394 Morogoro
MTEMI-maneno gani mnaambiana mbele yangu ?
NGANGANJIWA-Acha niwaambie hawa maana sijui wanagombania nini,wajukuu zangu
ACHENI KUGOMBANA (tamthilia ya kulogana)Kutunga japo baiti, uzito waniingia,
Nimeshindwa kusukuti, leo nawapasulia,
Kaniweza!
Kaniweza mtotongwa, kutunga sasa siwezi,
Ni dhahiri nimekwangwa, kanipitia mlozi,
Na akili nimefungwa, kwa ndumbaze na hirizi,
Kaniweza!
Kaniweza kila jambo, ya utunzi wa nudhuma,
Kunichukia mwajimbo, athama huku kuvuma,
Alianza na vikumbo, sasa majini katuma,
Kaniweza!
Kaniweza tena khasa, kwa wino wangu kumwaga,
Lakini ajuwe sasa, mwili naenda ukaga,
Zatosha hizi khamsa, sina budi kuwaaga,
Kaniweza!
25 Desemba 2017 Jumatatu 08:33am
Jina la Mtunzi Dotto Rangimoto
Jina la Utunzi Jini Kinyonga
Simu +255762845394 Morogoro
MTEMI-maneno gani mnaambiana mbele yangu ?
NGANGANJIWA-Acha niwaambie hawa maana sijui wanagombania nini,wajukuu zangu
1)Naona mnalumbana
Robo nusu kutukana
kwa magego mwaumana
mnataka kumezana
Ndita mwaangaliana
Sura mmekunjamana
kuna lipi la maana
Eti mnachezeana
mchezo wa kulogana
Mmeanza kutishana.
2)Kunani enyi mabwana
Kwanini kuna zozana
Uchawi kutupiana
Mnazidi daiana
Usiku mwachukuana
Angani mnapishana
Ubabe mwaonyeshana
Kwa vineno mwashindana
Sidhani mnajengana
Ndugu mnaboana.
3)Tungo mnapotezana
Ama mnataniana ?
Mlikwisha ambiana
Jifanye mwajitukana
Hilo twajichanganyana
Nona ndoto ya mchana
Ndugu wili kugombana
Wakti mlifundishana
Pale mlipokosana
Ni wajibu kupatana.
4)Kama toto mwafinyana
makonzi mwapigiana
Wote para mwanyoana
Na maji mshatiana
Ka duma mwakimbizana
Ohoo mnanyatiana
Bora mngelipatana
Na mikono kupeana
Atakavyo maulana
Ni haramu kugombana.
SHAIRI-ACHENI KUGOMBANA
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160
MBARU -ha ha ha ha ha ,huyoooo kajitaja
RANGI-nani
MKANYA-wewe,teh tehe tehe tehe
RANGI-(anainuka kwa hasira)ntakupiga wewe nimekwambia,nitakupigia,hunijui vizuri
MTEMI-kaa chini rangi,
Rangi anakaa chini kimya kinyonge
MTEMI-nani alikuwa shahidi kati yenu ?
MBARU-mimi hapa
MTEMI-Ulimioana nani anawanga ?
MBARU-sijui ila nilikuwa shahidi,nilishuhudia ila sikuwaona sura wote wawili
MTEMI-Ulishuhudiaje sasa ?
MBARU-Nilichanjiwa
watu wanashangaaa
SHETANI KATAJA JINA
Taireni wa viremba, wa hati na wa tunguli
Taireni nawaomba, mshike njia ya kweli
Msimchezeshe rumba, wala kumuweka mbali
Kutii amekubali, jina ametoa amba
Alivyojiona mwamba, kwa kutunisha misuli
Hali imeshamuwamba, hana lile wala hili
Atembea akiyumba, hana tena muhimili
Kutii amekubali, mtoeni hilo vumba
Chomboche juu ya mwamba, amevunja foromali
Tambo zote alotamba, na kujitia wakili
Maharage tano tumba, hulia kilo ugali
Kutii amekubali, atashika yenu kamba
Kule kujikombakomba, ulikuwa ujahili
Chungu ameshairamba, haya muavyeni seli
Mimi kaniita chemba, kaomba niseme hili
Kutii amekubali, msimchane msamba
Mtieni kwenye dimba, naomba mumsajili
Kesha maji ya uvumba, umwagiwe wake mwili
Kumuondoa magamba, asingwe kwa msandali
Kutii amekubali, mpokeeni wajomba
Mtunzi mwana wa Simba, jina Mbaruku Ali
Nimeamua kuamba, ndugu amaliza soli
Kuweni naye sambamba, twaeni yake kauli
Kutii amekubali, na msamaha kaomba
MBARUKU ALLY
MOTO WENU
0717199835
19:44
26/01/2018
Nikiwa Dodoma
Mzaliwa Moa Tanga
(watu wote wanatikisa vichwa kuashiri wameelewa)
MTEMI-kila mtu kaelewa au badoooooo ?
WATU-tumeelewaaaaaa
MTEMI-ombaneni msamaha
JUKWAA LINAZIMIKA TAA
nini kitaendelea............................................................?
SHAIRI-TAMTHILIA YA KULOGANA
MKUSANYAJI-Idd Ninga
WATUNZI-George Kyomushula
Dotto Rangimoto
Ibnu Mbaruk
Idd Ninga
Hamisi Kisamvu.
Ni story ya kubuni haina mahusiano na jambo lolote la kweli
imekusanywa na Idd Ninga,+255624010160 ,iddyallyninga@gmail.com

Post a Comment