Header Ads

test

Chocheeni-Mgorogoro wa Israeli na Palestina.





                 CHOCHEENI.

1)Alievuka mipaka,ya utu kwake hakomi
All na roho ya paka,hukomi wake ulimi
Kote hujenga viraka,kisa ni wake umimi
Endeleni kuchochea,na moto tieni kuni.

2)Mbaguzi kibaraka,shetani pia nyangumi
Mwenye nguvu na haraka,wengine kupiga ngumi
Kalaniwa yeye joka,ni kweli siyo uvumi
Endeleni kuchochea,moto gesi mwagieni


3)Subirini ukiwaka,dunia miaka kumi
Izidi sana bomoka,ukue wenu uchumi
Enyi mliopotoka,mkampinga Mtumi
Endeleni kuchochea,moto wake duniani.

4)Mbwa alolaanika,huosha USO kwa lami
One anasafishika,kwa simu akijihami
Gharika kwao lashuka,lipenye hadi Miami
Endeleni kuchochea,Dunia ife amani.

SHAIRI- CHOCHEENI
MTUNZI-Idd Ninga,Arusha
+255624010160.

Hakuna maoni