Header Ads

test

VITA BARIDI VYA MASHARIKI YA KATI -Ushairi Na Hisia

                               Pichani ni wanachama na wapenzi wa kundi la Arusha Poetry Club.



Kundi kuwa la wafia nchi walijikusanya katika uwanja wa vita kwa ajili ya kuanza vita vikali vya mashariki ya kati.
Vita vilivyoandaliwa kwa muda mrefu ili kumaliza mpambano wa kimaneno wa siku nyingi.
makamanda waote walikuwa tayari wameandaa vifaru na mabomu ili kuanza vita.
himaaaa himaaaaaa......
jeshi letuuuuuu.......
zilikuwa sauti za wapiganaji wakihamsha mori.
haya sasa kikosi cha mizinga kisonge mbele.....
kamanda alihamrisha  mashujaa wake wakae tayari kwa mashambulizi.
ghafla sauti toka mlimani ikasikika ikisema:


1)Washairi kulumbana,ni nani alianzisha ?
Washairi kugombana,lini tutatamatisha
washairi kuchukyana,jambo hili linatisha
Vya maneno vinachosha,vi vita vya washairi.

2)Washairi kupambana,jambo lisifurahisha
Washairi kuungana,itaja tufunganisha
Washairi kushikana,yaweza tuunganisha
Vya maneno vinachosha,vi vita vya washairi.

3)Washairi ndugu moja,mungu katukutanisha
Tushaikaneni pamoja,manenoya twangusha
Na subiri tukingoja,kabla kujitamkisha
Vya maneno vinachosha,vi vita vya washairi.

4)Washairi kupendana,babu alitufundisha
Washairi kuzozana,kuna mengi litafisha
Upendo na kupendana,nuru kutaiwakisha
Vya maneno vianachosha,vi vita vya washairi.

5)Kujiona ni mabingwa,ndiyo sumu twajilisha
Baraka zote zafungwa,kitungo nawajulisha
Kama balaa lajengwa,na miba tunajivisha
Vya maneno vinachosha,vi vita vya washairi.

6)Tushikaneni mikono,bila kujitenganisha
Tuviache vimaneno,vya weza tuchonganisha
Na kuleta malumbano,kisha kutupiganisha
Vya maneno vinachosha,vi vita vya washairi

7)Hovyo hovyo semeana,jambo hili lakondesha
Ni ya nini kupondana,ni maovu twaendesha
Tupendaneni kwa sana,sanaa kunenepesha
Vya maneno vinachosha.vi vita vya washairi

8)Kushaanza kulogana,tuhuma twazifurusha
Haya tena twatajana,zetu jina twaangusha
Hivi twavyofurushana,sifa zetu twachachusha
Vya maneno vinachosha,vi vita vya washairi

SHAIRI -VITA VYA WASHAIRI
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160

haya ni maji na tushayavulia nguo,nyinyi kina nani hadi mzuei vita vyetu,sisi ni mamwiji wa ardhi hii tutapigana mpaka mwisho wa dunia.......
 sauti ya kamanda inasikika akizungumza kwa hasira kali
vita vita vita vita vita vita.....
wanajeshi walisikika wakiimba .
 ghafla wingu zito linatanda angani,jua linazika ghafla  mwezi mchana unatokea.
wanajeshi wanaanza kutetemeka kwa hofu.
panaonekana kivuli kutoka angani kikishuka chini na kuimba kwa sauti ya upole

Kwa nguvuye ushairi,natema moto na radi
Vitu vilivyo hatari,iwapo sikujirudi
Unidhanie amiri,mahali penye junudi 


Kutoka kielelezo cha fasili
Shaaban bin Robert(1968)
Ukurasa 21

wingu linapotea na hali ya kwaida inarudi.
ndiooooo huu ni uoga wetu hakuna kitu hapa.......kamanda anasema kwa kujidai
tusitishike hizi ni dali za sisi kushinda vita.....shujaaa mmoja anasema lakini akionekana kuogopa.

Mwanajeshi mmoja aliekuwa tayari amebeba silaha yake ya kirusi maarufu kama a.k.a 47 anakamatia bundiki huku akiwa amepiga magoti mbele ya wanajeshi wenzake na kuwaambia

Shaha Bola Kiburi utanguliza, maangamizi makuu
Mashindano yachukiza, usione kwenda juu
Letu kujinyenyekeza, twajua mwenye ukuu

Mizozano yaumiza, muhali ona nafuu

                                                                                             Shaha Bola
                                                                                                                SHAHA BOLA
toka  toka tutakupiga risasi,wewe ni si shujaa wewe ni muoga sana......mwanajeshi mmoja anamvuta kwa hasira nusura ampige.
wenzake wanamkimbilia na kumshika.

triiiiiii puuuuuu paaaaaa triiiiiii paaaaaa.........sauti ya radi inapiga huku jua likiwa linawaka'
tukimbieni hapa tutakufa...... shujaaa mmoja anaonekana akikimbia huku baadhi wakimfuata.
wanajeshi wengine wanabaki kutulia kikakamavu kwani kulingana la sheria za jeshi lao hawaruhusiwi kukimbia.
katika kati yao panatimka vumbi kubwa linaloziba macho yao na anaonekana kama mtu kutoka katika vumbi hilo akisema:


           VITA VYA WATUNZI.
Mi malenga mpekuzi,na pia mwana mchina.
Majina haya ya kazi,muyajue kwa bayana.
Hubi wangu laazizi,huniita wake mwana.
Sote tutafuatana,kiswahili kukienzi.
Watunzi wa zile enzi,jamani walipendana.
Tena walikuna nazi,mtini walikutana.
Haki hawakuwa wezi,kwa tungo kuibiana.
Sote titafuatana,kiswahili kukienzi.
Hawakuwa wabeuzi,na hawakuchukiana.
Walikuwa moja ngozi,ili kushirikiana.
Ndipo nawapa pongezi,kazi yao ya maana.
Sote tutafuatana,kiswahili kukienzi.
Hadi leo hata juzi,watunzi wanapendana.
Na wenzao hawambezi,wanawatunza vijana.
Watunzi si wanyakuzi,nudhuma kunyakuana.
Sote tutafuatana,kiswahili kukienzi.
Na lugha waliienzi,ngeli wakachambuana.
Maovu walihirizi,kweli waliteteana.
Walitufunza malezi,tena yalo bora sana.
Sote tutafuatana,kiswahili kukienzi.
Wale wa sasa washenzi,wanaeneza fitina.
Wanatutia ajizi,usiku hata mchana.
Kweli hili ni simanzi,watunzi tuna laana.
Sote tutafuatana,kiswahili kukienzi.
Yananitoka machozi,ninaumiya mchina.
Kuona vile watunzi,heshima kuvunjiana.
Hata wapikapo mbizi,hadhi wanashushiana.
Sote tutafuatana,kiswahili kukienzi.
Nawambia waziwazi,tuishi tukipendana.
Tulishane hata ndizi,kwa begani kushikana.
Waswahili waokozi,shida wanaokoana.
Sote tutafuatana,kiswahili kukienzi.
Msinione mchizi,nipotimamu mchina.
Hewani tutabarizi,Diani tukikutana.
Ninaondoka wapenzi,nawaacha kwa Rabana.
Sote tutafuatana,kiswahili kukienzi.
Malenga Mpekuzi.
Abdulhafit M Farah.
#mwana_mchina.
COUNTY HIGH SCHOOL-GARISSA.
   anapotea kusikojulikana.
nini hiiii.........
au labda tumekuja kupigana katika uwanja wenye laana......
hapana hapa kutakuwa kuna mchezo wa mazingaombwe tunafanyiana........ kamanda mmoja anajiuliza na kujijibu mwenyewe.
 mwanajeshi mmoja anwasha gari lake,anakimbia na kwenda kukaa mbali na wenzake anawaambia:

                        MWUNGWANA SINENI.
Mungwana ninene nini,yeshanenwa ya kunenwa,
Palishanenwa zamani,'mema yalishatafunwa',
Kimya changu mdomoni,ingali vazi lachanwa,
Sitanena yalonenwa,la kufa halina dawa.
*
Mwungwana akichutama,aibu humuepuka,
Kahofia kusimama,ya utupu kuoneka,
Aliyejipa kilema,habathi alojitwika,
Sitanena yalonenwa,la kufa halina dawa.
*
Ngoma ikivuma sana,husikika mpasuko,
Alowamba ngoma jana,kasababisha mauko,
Matao hayako tena,tamu ya ngoma haiko,
Sitanena yalonenwa,la kufa halina dawa.
*
Inaonekana nuru,nuru yaliwa na kiza,
Waja tuliidhukuru,tahamaki yatuliza,
Tulitaraji shukuru,leo tunaomboleza,
Sitanena yalonenwa,la kufa halina dawa.
*
Wa kutufuta machozi,sababuye tunalia,
Ile yetu mun'tazi,kimako twaimakia,
Inachuna zetu ngozi,wangwana tunaumia,
Sitanena yalonenwa,la kufa halina dawa.
                          Ally Sufiani,
                          Tanzania.
hivi vita mimi siviwezi piganeni wenyewe,mimi narudi zangu nyumbani......mwanajeshi huyo anasema


 Yalo nenwa usinene,bora uwe jito toko!
Uziepuke senene,na mangi mahangaiko
ishima muekeane,na udugu wa mashiko!

Halina dawa lakufa,usiambe yaloambwa!

                                                                                                                Abu-Bakari Jabu Salim 




                 KUNANI?
Sijui anga ninjozi,au ni hali halisi....
Mananeni usingizi,hivi hivi najihisi..
Au kelele zajuzi,zisonipa usingizi!
NAUZA KWANI KUNANI,WASHAIRI WALUMBANA!
@
Nikasikiza vizuri,ni upepo nayo kusi..
Wavuma sivyo vizuri,uvumavyo unakasi..
Nikawasha kibatari,kwa wingi wa wasi wasi.
NIKIYAUZA VIZURI MALUMBANO YA CHIBERO!
@
Kitandani sikutuwa,pole nikapajilisi....
Mara ikaanza mvuwa,kibarabando nakusi.
Hapo ndipo nilijuwa,mkubwa mola qudusi.
KUNANI NIKIYAUZA KILA KONA NI MATUSI!
@
Moyo ukawa wadunda,mbio mbio nadadisi.
Ino ndio parapanda?kiama chaja upesi.
Mbona nipo njia panda,yarabi nipa wepesi
NIKIUZATO NI NINI NIULUMBI WAUSHINDI!
@
Kusi yaja kwa gharika,mvua nayo mwendo kasi.
Huku ninabagarika,baridi juu utosi....
Gafula nikagutuka,haraka tena upesi
NIKIJARIBU KUUZA,HAKUNA ANOELEWA!

                                              MTUNZI-Mzora Swalehe

Apigweee apigweee,apigwe huyo apigwe.............. wanajeshi wa pande zote mbili wanaanza kuokota mawe na kumrushia mwenza....

JE NINI KITAENDELEE.....USIKOSE SEHEMU YA PILI

MKUSANYAJI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com

vWATWWW
WATUNZI:
                  Idd Ninga
                 Shaha Bola
                 Abuu Bakari Jabu Salamu
                Abdulhafit De Speaker
               Mzora Swalehe
               Ally Sufiani

Hakuna maoni