Header Ads

test

KYOMUSHULA LAZIMA UOE TU,TAKA USITAKE













           KYOMUSHULA OA
1)Kuoa jambo la kheri,Joji ninakuusia
kuoa ni ufahari,mke utajivunia
Michepuko kweli shari,hilo ninakuusia
Kyomushula sasa oa,acha mambo ya kihuni....

2)Acha mambo ya kihuni,motoni utaingia
wewe ni mtu wa dini,vipi ndoa wakimbia
unaishije mjini,mke hujajipatia
Kyomushula sasa oa,ndo hitokufilisi.

3)Ndoa hitokufilisi,raha utajionea
Acha tamaa ya fisi,huku kule kurukia
Oa upande farasi,ona utavyonukia
Kyomushula sasa oa,kwishi mwenyewe ushamba.

4)kwishi mwenyewe ushamba,mchumba twakupatia
mnene pia mwembamba,mrembo anavutia
Hakika mungu kaumba,ukimwona hutolia
Kyomushula sasa Oa,ufurahie maisha.

5)Ufurahie maisha,mahari twakulipia
Yote hadi inaisha,gharama twagharamia
Ndoa twataka fundisha,huto toa hata mia
Kyomushula sasa Oa,usiogope maisha.

6)Usiogope maisha,Azaza alinambia
Mke tamsafirisha,tikite kamkatie
Ya ndege toka Arusha,hadi Dar akitua
Kyomushula sasa oa,umri unazidi kwenda.

7)Umri unazidi kwenda,miaka inasigea
Siyo kwamba nakuponda,ila tumeshagundua
Episii twakupenda,harusi twakwandalia
Kyomushula sasa oa,ole wako ukatae.

8)Ole wako ukatae,fimbo tutakushikia
Mke uje kaa nae,nguo akikufulia
Vingine ujivunie,mwenyewe utajonea
Kyomushula sasa oa,tena mtoto wa jeshi.

9)Tena mtoto wa jeshi,mafunzo amepitia
Mpole pia mcheshi,maadili anajua
Mtalamu wa mapishi,vitu akikupikia
Kyomushula sasa oa,mikanda hatokupiga.

10)Mikanda hatokupiga,kama ukimchezea
Vibaka wakikutega,ataja kukutea
Kama ukilega lega,vingi atasimamia
Kyomushula sasa oa.usisubiri mihela.

SHAIRI-Kyomushula oa
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
iddallyninga@gmail.com
+255624010160
See More

Maoni 1 :