Shairi-Kheri na Shari
KHERI NA SHARI
Palipo dhiki na tabu, matatizo na michosho
Maisha yenye adhabu, shida na mihangaisho
Hapo kunalo jawabu, kheri nayo suluhisho
Katika tumbo la shari, ndimo inakaa kheri.
Ja zinduna na ambari, zilivyobeba fundisho
Vinavyokwenda sanjari, kama bibo na korosho
Jua hakuna hatari, isiyo salama mwisho
Katika tumbo la shari, ndimo inakaa kheri.
Mshairi Machinga,
mfaumehamisi@gmail.com,
+255716541703/752795964,
Dar es salaam, Kkoo.
Post a Comment