Header Ads

test

Lugawa

 


Shairi hili limeandikwa na:
HAMIS A.S. KISAMVU
  0715311590
  kissamvujr@gmail.com
  Baitu shi'ri- Mabibo
          Dar es salaam - Tanzania
02-feb-2023


Nafusini nina hawa, via vyanipa tatizi,
Zimedhofu zangu mbawa, hazi himiri vuvuzi,
Kuruka mbali siwezi, dhaifu mie Lugawa,

Sijui kama tu sawa, Kipungu nawe Kisozi,
Mwenzenu nimehemewa, zanitatiza pumzi,
Kuruka mbali siwezi, dhaifu mie Lugawa,

Mwendapo sijapajuwa, safari hamnelezi,
Nahofu kuwasumbuwa, kwenye yenu matembezi
Kuruka mbali siwezi, dhaifu mie Lugawa,

Hapano nilipokuwa, hatua siziongezi,
Tachopata majaliwa, kanijalia mwenyezi,
Kuruka mbali siwezi, dhaifu mie Lugawa,

Siwezi kwenda kutuwa, mbali na yangu makazi,
Kwa ninyi kunizuzuwa, tapata usaidizi,
Kuruka mbali siwezi, dhaifu mie Lugawa,

Mungu ndiyo katugawa, naifanyaje ajizi,
Dudumizi ukiwa, ya Kipanga huyawezi,
Kuruka mbali siwezi, dhaifu mie Lugawa,

Tama nataka afuwa, isiyonipa chagizi,
Itonifanya kukuwa, kama mche na mizizi,
Kuruka mbali siwezi, dhaifu mie Lugawa,

Hakuna maoni