Header Ads

test

Matumizi sahihi ya 'AMPASENDI ' (&) inayowakilisha "NA" katika lugha,sehemu ya pili.


Mudhihir  S. Njonjolo muandishi wa makala hii.


MATUMIZI SAHIHI YA AMPASENDI(&)INAYOIWAKILISHA "NA" KATIKA LUGHA.SEHEMU YA PILI.

Pichani,ni mtaalamu wa lugha na mwandishi wa hadithi nchini Marekani anayeitwa Patrick James Rothfuss.Ni mwandishi wa zama zetu hizihizi.Kazaliwa tarehe 6 /6/1973.Ni mwandishi wa kitabu maarufu na mashuhuri sana kiitwacho "The Name of the Wind".Nimemtanguliza kabla ya mwendelezo wa somo letu kwaajili ya kuyakumbuka maneno yake kadhaa alowahi yaandika kuhusu uzito na nguvu ambayo "lugha" imeumbiwa nayo. Alisema ambavyo kwa Kiswahili inaweza kueleweka hivi hivi,
"Maneno ni vivuli vilivyofifia vya majina yaliyosahaulika.Kama ilivyo kwa majina,yana nguvu(maneno).Maneno yanaweza kuwasha moto katika akili za watu.Maneno yanaweza kuzibua machozi katika nyoyo zenye ugumu".




Patrick James Rothfuss.


Si kwa lolote lingine kuyanukuu maneno hayo,ila kwaajili ya kuzibua mapenzi ya kusoma kwa nyoyo zilizo ngumu na vivu kushughulikia kila palipo penye andiko.

1.Tumia ampasendi(&) katika "shorthand expressions".Ni maandiko ya haraka haraka ambayo hufanywa kwa kufupishwa au kuwekwa alama kutokana na kuokoa muda katika maandishi au nafasi kutotosha.Ni kinyume cha huu utaratibu wa kawaida wa kuandika ambapo hutumiwa "longhand".Katika "shorthand",yaani kufupisha,lengo litakuwa kuokoa nafasi,basi huitwa "Stenography",itokanayo na lugha ya Kigiriki yaani "stenos" kwa maana ya "narrow" ambayo ni "wembamba" na "graphein" ambayo husimama kwa ajili ya "to write" yaani "kuandika".Pia huitwa wakati mwingine "brachygraphy" kutokana na neno la Kigiriki "brachys" ambayo ni "short" katika Kiingereza yaani "kufupisha".Lakini kama ni kwa shauri ya muda ndio maana hufupishwa maandishi haya,basi itakuwa inaitwa "tachygraphy" kutokana na neno "tachys" ambayo husimama kwa maana ya "spidi".Kwahiyo katika mazingira haya ndipo unaweza kutumia ampasendi ili kuokoa nafasi au muda katika maandishi.
Kwa mfano.(R & D) husimama badala ya "Research and Development" na ni maarufu au ya kawaida"common" duniani kote. Lakini pia badala ya kusemwa "Dkt.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu",basi inawekwa tu pale (JPM & WM/PM)halafu yaendelea  safari ya kuandika.

2.Hutumiwa ampasendi katika orodha ambayo hii "na" yenyewe iko sehemu ya kile kinachoorodheshwa.Mfano.Kuna orodha inatolewa ya makala bora Afrika.Lakini katika jina moja la makala lina sehemu mbili zilizounganishwa.Baada ya kutajwa makala zingine,kisha ikaja makala ya Mh.Samia Suluhu Hassan ambayo inaitwa "Kavu na Mbichi".Kwahiyo kinapatikana kitu kama hiki hapa yaani vichwa tofauti tofauti vya hizo makala,"Bombardier,Treni  ya Umeme,Uwajibikaji,Ufuatiliaji,
Kavu & Mbichi,".

3.Hutumiwa ampasendi(&)katika majina ambayo yenyewe tu ni vifupisho.Kwa mfano.(AT&T).Lakini kumbuka kuwa hapa huiwachii nafasi ampasendi ila utaibana kama kawaida.

4.Hutumika ampasendi katika kunukuu marejeo ya waandishi wa Kitaaluma.Mf.(Njonjolo,Aljanean,Kivuyo,Kiango  & Massamba, 2020).Na hii ni kwa mujibu wa "American Psychological Association" au (APA).Lakini kwa mujibu wa "Morden Language Association of America" yaani "The MLA Style Manual" na "Chicago Manual of Style" wao husimamia katika kutumia "and" au "na" tu sehemu hii badala ya ampasendi (&).

5.Hutumiwa katika kutambulisha waalikwa wawili. Yaani inasemwa kama (Bw. & Bi).

6.Mwisho,ampasendi kutumika katika kuwakilisha "etcetera" au "and so forth" yaani "n.k".Kwa sasa inatumika maarufu "e.t.c" lakini inafaa kufupisha na ikaandikwa "&c" na itamaanisha "e.t.c".

Huu ni mwisho wa matumizi ya alama ya ampasendi,na tukutane tena wakati mwingine katika somo letu la "Writing Mechanics".

Mudhihiri S.Njonjolo.
Mtwara-Mjini.
20/5/2018.

Hakuna maoni