Kumbukumbu ya Lucky Vicent.
1)Nayakumbuka majonzi,yalotokea Arusha
Wengi wao wanafunzi,kifo kilitukumbusha
Mwenyezi alomjenzi,ndie ataetufisha
Ulikuwa ni msiba,uloshitua taifa.
2)Watu waligaragara,machozi yakawatoka
Haikuwa masikhara,vilio vilisikika
Vichwa vikakosa dira,ajili kuvurugika
Ulikuwa ni msiba,uloshitua taifa.
3)Na wale walo na presha,waliiaga dunia
Kifo kiliwaangusha,bari waliposikia
Ni tukio la kuitisha,ngumu kulisimulia.
Ulikuwa ni msiba,uloshitua taifa.
4)Wengine waliumia,wakabaki walemavu
Machungu walisikia,na makali maumivu
Kwa uchungu walilia,zikabana zao mbavu.
Ulikuwa ni msiba,uloshitua taifa.
5)Katu hitosaulika,watu walivyoumia
Machozi yaliwatoka,na wengine kuzimia
Na chini walidondoka,nguvu zikawaishia
Ulikuwa ni msiba,uloshitua taifa.
6)Tulienda waombea,kwenye nyumba za ibada
Kifo chatukaribia,huja bila ya ziada
Kifo hajali hajali hatia,kifo hasubiri ada
Ulikuwa ni msiba,uloshitua taifa.
7)Lucky Vicenti shuleni,mayowe yalisikika
Hakuna aloamini,tarifa ilipofika
Damu ndogo masikini,tayari ziliyoweka
Ulikuwa ni msiba,uloshitua taifa.kwa
Hata singeliambia,ngejua kuna kilio
Haiwezi kupotea,kumbu ya hili tukio
Ulikuwa ni msiba,uloshitua taifa
SHAIRI-KUMBUKUMBU YA LUCKY VpICENT
MTUNZI-Idd Ninga,Arushayani
+255625010160
iddyallyninga@gmail.com.
Post a Comment