Header Ads

test

Choper Machepe adaiwa kuiba wimbo wa CHAPA ILALE,na kuifanyavyake




Choper a.k.a Choper Machepe.

Changamoto ya ulinzi wa kazi za Sanaa bado imekuwa ngumu na nzito kwa wasanii wa changa na wakubwa kufuatia Tuhuma za Mara kwa Mara za wasanii kuibiana nyimbo.
Wizi wa kazi za wasanii umekuwa ukifanyika katika kila tasnia hata ya Ushairi pia.
Choper machepe ni msanii chipukizi toka jiji la utalii la Arusha ambae aliwahi tamba na kibao chake "kachubwichu" kabla ya kuja kutoa kibao kingine kipya kinachotamba sasa kwa jina la "Chapa Ilale" ambacho kimeingia katika mzozo na wasanii wenzake wawili ambap wote wanadai kuwa wao ndio waandishi wa nyimbo hiyo ambayo walipanga kushirikiana wore watatu kabla ya Machepe kuwazunguka wenzake  na kuitoa nyimbo hiyo peke yake chini ya Mensen selecta.

Dulla S,mtayarishaji wa muziki anaedae kuandika wimbo wa "chapa ilale"

Msanii Dulla S ambae ni muandaji wa muziki alidai kuwa yeye ndie alieanzisha wazo la kutoa nyimbo ya chapa ilale ambae ni kisingeli cha kwanza kutoka mkoa wa Arusha kutamba redioni.
Dulla D amedai nusu ya nyimbo aliandika yeye na baadae alimshirikisha msanii Mbosso Tz kutoka Dar es salaam ili kuongezea maneno Baadhi ya maneno katika wimbo huo.
Dulla S anadai kuwa waliamua kumuita Choper baadae ya Choper mwenyewe kuomba kushirikishwa katika nyimbo hiyo na Dulla alikubali kwa kuwa tu Choper ni msanii Mwenzake toka Arusha.



Mbosso Tz,aloshiriki kuandika wimbo wa "chapa ilale"

Msanii Choper baada ya kupata mashairi yote ya wimbo huo ndipo alipoamua kwenda kumchukua msanii mwingine maarufu kama Almando toka kundi la jambo squard na kurekodi wimbo huo bila kuwataarifu wenzake.
Dulla S anasema alishangaa kuona wimbo aloandika kwa mikono yake ukiimbwa na mtu bila idhini yake.
Dulla S amesema kuwa kwa sasa anajiandaa kuchukua hatua ikiwemo kupeleka malalamiko kwa Mensen selekta ambae alisimamia kazi hiyo.
Dulla S pia amesema mbali na hivyo amejaribu pia kumpigia Machepe simu lakini amekuwa akikata ama kutoipokea kabisa.

Hakuna maoni