Pumzika Kwa Amani Tambwe Hiza
Hakuna myongoni mwetu,kitakae mbakiza
Kifo ni kivuli chetu,nasi kipo twatembe
Pumzika kwa amani,Richad Tambwe wa Hiza.
2)Mauti ndie mlangio,nawe umeshaingia
Mauti kama mchango.sote tutauchangia
Mauti hayana hongo,eti tukayakimbia
Pumzika kwa amani,Richad Tambwe wa Hiza.
3)Tambwe umetangulia,na sisi tunafwatia
Chadema ya kulilia,na yako famili pia
Kifo ndio yetu njia,sote tutakipitia
Pumzika kwa amani,Richad Tambwe wa Hiza.
4)Tambwe mwana harakati,nchi kuipigania
Kasi kusini na kati,kule ulifikiria
Na kupanga mikakati,maendeleo
Pumzika kwa amani,Richad Tambwe wa Hiza.
5)Kwa moyo kwa kijasiri,gari ulijiwashia
Hukujua ya kujiri,kifo cha kukaribia
Hakika kumbe tayari,saa imeshafikia
Pumzika kwa amani,Richad Tambwe wa Hiza.
6)Kazi yako duniani,tayari imetimia
Twakombea kwa manani,pema kupumzikia
Fikra zako jukwaani,sote tutazienzia
Pumzika kwa amani,Richad Tambwe wa Hiza.
SHAIRI -TAMBWE HIZA (R.I.P)
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160
Post a Comment