Joto Lazidi Kupanda
1)Huyu hataki utani,vyema mumchagueni
Ilikuwa kampeni,alisema jukwaani
Faraja i sandukuni,na kura zenu mpeni
Vipi mbona mnalia,joto lazidi kupanda.
2)Yule anacheka cheka,mkamfanya mtani
Wengi mkaanza deka,na kutamba mtaani
Chukua unachotaka,atakuuliza nani
Mbona mnalalamika,joto lazidi kupanda.
3)Maswali mnaulizwa,vipi mnaenda chini
Tadhani utaulizwa,kama ilivyo zamani
Bakora inatembezwa,vumilieni jamani
Naona mnazimia,joto lazidi kupanda.
4)Walozoea kunyonga,leo wakabwa kooni
Tabia ya ukipanga,yawatokea puani
Nahisi wanajipanga,wakimbie kanisani
Mbona mnateteana,joto lazidi kupanda.
5)Mafisadi sasa chali,kuiba hawatamani
Watetema yao hali,na vijasho vya kwapani
Amewashika jabali,hali nghumu si utani
Waropokaji mu wapi,joto lazidi kupanda.
6)Moto wazidi waka,sasa machozi ya nini
Jamaa analipuka,kutumbua hadharani
Si wenyewe mlitaka,mwalalama kulikoni
Matumbo yatikisika,joto lazidi kupanda.
SHAIRI - JOTO LAZIDI KUPANDA
MTUNZI- Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160
Ilikuwa kampeni,alisema jukwaani
Faraja i sandukuni,na kura zenu mpeni
Vipi mbona mnalia,joto lazidi kupanda.
2)Yule anacheka cheka,mkamfanya mtani
Wengi mkaanza deka,na kutamba mtaani
Chukua unachotaka,atakuuliza nani
Mbona mnalalamika,joto lazidi kupanda.
3)Maswali mnaulizwa,vipi mnaenda chini
Tadhani utaulizwa,kama ilivyo zamani
Bakora inatembezwa,vumilieni jamani
Naona mnazimia,joto lazidi kupanda.
4)Walozoea kunyonga,leo wakabwa kooni
Tabia ya ukipanga,yawatokea puani
Nahisi wanajipanga,wakimbie kanisani
Mbona mnateteana,joto lazidi kupanda.
5)Mafisadi sasa chali,kuiba hawatamani
Watetema yao hali,na vijasho vya kwapani
Amewashika jabali,hali nghumu si utani
Waropokaji mu wapi,joto lazidi kupanda.
6)Moto wazidi waka,sasa machozi ya nini
Jamaa analipuka,kutumbua hadharani
Si wenyewe mlitaka,mwalalama kulikoni
Matumbo yatikisika,joto lazidi kupanda.
SHAIRI - JOTO LAZIDI KUPANDA
MTUNZI- Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160
Post a Comment