Header Ads

test

DARASA LA MAFAHALI



          DARASA LA MAFAHALI
Mkononi nashika chaki,utao nauandika
Siyo kama mi sitaki,mloto unasomeka
Na vaa vazi la kaki,ukwapi unazinduka
Mtamu usi na dhiki,kama pindu kaumbika
Darasa la mafahali,makomando jemedari.


tuwaache halaiki,kikwamba kikisifika
Kisishika mamluki,kwa vina visivyonuka
Tasdisa si falaki,ulogwe ukalogeka
Mandhuma kama laki,msuko ukipangika
Darasa la mafahali,makomandi jemedari.


mloto kama mkuki,mleo hautazika
Mkarara huchomoki,mwandamo ukilipuka
Kibwagizo chenye keki,ubeti ukichezeka
Takhmisa huandiki,kisa kili imechoka
Darasa la mafahali,makomando jemedari.








ukumi tungo ya haki,kamwe hitofurahika
Wote wala mishikaki,mafisadi wang'atuka
Mavue kumaliziki,tungo nzuri tengezeka
Wawe asili ya nyuki,katujalia rabuka.
Darasa la mafahali,makomando jemedari.




tenzi nzuri zihakiki,ukawafi ukishika
Sama bila ya mikiki,haiwezi kufutika
Kibwagizo si fataki,eti boma kulipuka
Talthitha huzinduki,soma uje furahika
Darasa la mafahali,makomando jemedari.


kwa bahari pasifiki,inkisari punguzika
Tabdila wako rafiki,mandhuma si dhihaka
Ukaraguni iliki,na shairi linalika
Guni vue zi lukuki,kichwani zitochanika
Darasa la mafahali,makomando jemedari
mtunzi wa shairi la DARASA LA MAFAHALI
Idd Ninga







Hakuna maoni