Header Ads

test

Hekima ya Bi Mkali

 



Wasaa umetimu, kaa kitako sikimbie,
Msijivike wazimu, ghafla mnivimbie,
Weka chini hiyo simu, hekima niwaambie,
Sikiza Hizi hekima, hekima za Bi.Mkali!

Bi.Mkali alienda Beijing, mkutano wa wanawake,
Sio kujifunza Tai wala Ching, ama kurusha teke,
Kajifunza Queen ni King, ila asiye na makeke,
Sikiza Hizi hekima, hekima za Bi.Mkali!

Haya! Basi Bi.Mkali anena, anena tena nawe,
Mabinti sharti shirikiana, sio kutupiana mawe,
Vyeo mnashushana, wafaidikani nawe?
Sikiza Hizi hekima, hekima za Bi.Mkali!

Bi.Mkali awapasha, na hekima azitoa,
Uwezo wako onesha, sio nguo kuzitoa,
Vidonda vyao ponesha, kesho watakutoa,
Sikiza Hizi hekima, hekima za Bi.Mkali!

Namalizia sasa, nanyi wanaume,
Usawa ndo usasa, fursani KE tuwatume,
Kuwapa vyeo yatupasa, maendeleo wasukume,
Sikiza Hizi hekima, hekima za Bi.Mkali!

Equality and equity, MUST be promoted,
It's the quantity and quality, should be sorted,
Femininity solidity, inferiority? Never escorted
Women!You are the now & the future presidents!
Sikiza Hizi hekima, hekima za Bi.Mkali!

Mtunzi: Naamala Samson
+255 716 748 674

Hakuna maoni