Header Ads

test

Moyo Wangu Tulia


 




Sitaki tena sitaki,moyo wangu usumbuke
Sitaki nipate hiki,rohoni nihangaike
Sitaki nipate kiki,wa jamii wanicheke
Moyo wangu we tulia,mjini kuna vya watu.

Moyo wangu funga macho,vya watu visikuteke
Penda hiki ulonacho,rohoni uburudike
Chako pekee kificho,ndo bahati ubahatike
Moyo wangu we tulia,mjini kuna vya watu.

So kwamba ninaogopa,ila heshima nachunga
Leo pale kesho hapa,hilo jambo la kijinga
Moyo hutotoka kapa,tulia ile mpunga
Moyo wangu we tulia,mjini kuna vya watu.

Acha niunde vya kwangu,ili vije kupendeza
Niseme hivi ni vyangu,vile nilotengeneza
Vilivyo chaguo langu,si hivi vya kunguza
Moyo wangu we tulia,mjini kuna vya watu,






Hakuna maoni