Header Ads

test

Futari ya Israfu






            TUACHE ISIRAFU.

1)Wapo wanakula sana,wafuturu kwa haraka
Leo twalinganiana,chakula kiwe haraka
So kwamba twasema,tusije kukasirika
Tuacheni isirafu,Tufuturu kawaida.

2)Mtu wafuturu sana,kama daku hutokula
Tambi na uji wa dona,kwa wingi wafanya hila
Wafikiri hiyo suna,ama kisa una hela 
Tuacheni isirafu,Tufuturu kawaida


3)Tende halua viazi,wala kama wafukuzwa
Tumbo huliachi wazi,ama wataka kukuzwa
Hata marage ya Nazi,wala kama unauzwa
Tuacheni isirafu,Tufuturu kawaida.

4)Vyakula vingi kwa wingi,wafuturu peke yako
Wapiga futari nyingi,na kusahau wenzako
Huo si wetu msingi,litavimba tumbo lako
Tuacheni isirafu,Tufuturu kawaida.

5)Ama walipa kisasi,cha kutokula mchana
Basi sasa sema basi,njaa Kali mimi sina
Hadi wakua mweusi,kula kama wapigana
Tuacheni isirafu,Tufuturu kawaida.


6)Futari nyingi washiba,hadi wasindwa kuswali
Tumbo wafanya kibaba,wawa taabani hali
Funga igeuze tiba,afya yako wewe jali
Tuacheni isirafu,Tufuturu kawaida.

SHAIRI -TUACHE ISIRAFU
MTUNZI-Idd Ninga,Arusha
+255624010160


Hakuna maoni