Header Ads

test

Ushairi ni mgumu kuliko muziki

Ramadhani Juma ama kama kama anavyojulikana kwa jina la kisanii Rama C Chenay ni chipukizi wa muziki wa kizazi kipya maarufu kwa jina la bongo fleva ambae alianzia safari yake ya kimuziki akiwa mkoani Arusha na baadae kuhamia mkoani Dar es salaam ambako anaendeleza kazi zake hadi sasa huku akifanya kazi katika studio mbalimbalio huku kubwa kabisa ni ile ya mtayarishaji muziki maarufu nchini Mr Touch.
Rama C Chenay alianza Arusha katika studio za Baefoot Record za mtayarishaji Justino ambako baada ya  kuona kuwa anahitaji kubadili mazinghira ya kikazi Rama C aliamu kwenda Dar es salaam ambako alijiunga na kundi la msanii mmoja mkubwa lakini muda mfupi baade walitengana kutokana na matatizo ya kimuziki ambayo siyo vyeam kuyataja hapa kwa kiwa sijafanya mahojiano na woten wawili na pia lengo langu siyo kuandika  matatizo ya wasanii wa kimuziki.
Nilibahatika kuzungumza nae msanii huyo mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya mahusiano katika ya muziki wa kizazi kipya na kazi ya  ushairi.
Rama C Chenay amekiri ya kwamba muziki ni mrahisi kuliko utungaji wa mashairi,na haya ndio maneno yeke;
NILIANZA KUJIFUNZA SANAA MBALIMBALI NIKIWA MKOANI ARUSHA,NILIJIFUNZA KUIGIZA MICHEZO YA JUKWAANI NA ILE YA FILAMU,NILIJIFUNZA HUHARIRI WA VIDEO AMBAO NAENDELEA NAO HADI SASA,NILIJIFUNZA UPIGAJI PICHA WA VIDEO,LAKINI NILIPOJIFUNZA USHAIRI ILIKUWA NGUMU SANA,NILITUMIA MUDA MWINGI KUJIFUNZA MASHAIRI YA KIMAPOKEO LAKINI NILIFELI,MUZIKI NI MRAHISI SANA JAPO UNACHANGAMOTO LAKIN I USHAIRI NI MGUMU KULIKO,ACHA NISEME UKWELI,WASHAIRI WANATUMIA AKILI NYINGI KATIKA KUTUNGA,WANAMUZIKI HATUJALI VITU VINGI KATIKA UANDISHI WA MUZIKI WETU,HATUJALI VINA WALA MIZANI,TUNAWAZA KUIMBA TU ,LAKINIWASHAIRI WANAWAZA JINSI YA KUUNDA MASHAIRI YAO NA WANAJUA KUPANGILIA VINA NA MIZANI TOFAUTI NA SISI WANAMUZIKI,JAPOKUWA KUNA BAADHI YETU TUNAITA MUZIKI WETU MASHAIRI LAKINI KWA MAONI YANGU NI LAZIMA TUESHIMU VIPAJI VYA WAETU WENGINE,HATUWEZI JISIFU NA SISI NI WASHAIRI HALI YA KUWA HATUWEZI WALA KUZINGATIA KANUNI ZA USHAIRI WAO,UKWELI USHAIRI NI KAZI NGUMU,JAPO NATAMANI SANA KUUJUA.

 Rama C anasema anatamani sana kujifunza ushairi ili kuongeza ujuzi katika muziki wake ila anapata changamoto sana katika kupata watu wa kumfundisha sanaa ya ushairi kwani kwa Dar es salaam hajaona kundi la sanaa linalofundihs amashairi kama ilivyokuwa Arusha kwa kipindi cha mwaka 2013.
Rama C Chenay mbali ni kuimba muziki pia ni mpiga picha katika kampuni yake ndogo ya utayarishaji wa video ijulikana kama RAMA C PRODUCTION na yeye hufanya kazi kama muongojazi wa video katika kampuni yake.
Rama C anasema yupo tayari kufanya video za washairi ambao watakuwa wapo tayari kufanya nao kazi kwani malengo yake makubwa ni kuona sanaa ya ushairi inasonga mbele hata kama hana uwezo wa kuandika wala kutunga mashairi mashairi lakini anapenda snaa hiyo ya ushairi iwe juu kama zilivyo sanaa nyingine.
Amesema licha ya kwamba yey ni msanii asiejulikana lakini haitomvunja moyo wa kuendelea kufanya sanaa yake. 




Hakuna maoni