Choper Machepe atamba vyema na wimbo wa CHAPA ILALE
Mkoa wa Arusha ni mkoa pekee ulojaaliwa kuwa na vijana kwenye vipaji tofautitofauti ambao Mara nyingi vijana katika mkoa huu wamekuwa wakitumia juhudi na maarifa katika kuhakikisha wanaitangaza na kufanya vyema sana ya mkoa huu.
Vijana wengi wa JIJI la Arusha na Arusha kiujumla wamekuwa ni wabunifuna wa chapa kazi katika kuhakikisha hawabaki nyuma katika ukuzaji wa kazi zao.
Unapoongelea Sanaa ya Arusha njua unaongelea sanaa tofauti tofauti zinazo fanywa na vijana wa hapa bila ya kuzingatia rika lao.
Chopa machepe ambae kwa siku zilozopita tuliandika habari ya sakata lake la kutuhumi na muandaaji wa muziki Dulla S kuwa aliiba wimbo wa CHAPA ILALE lakini baada ya uchunguzi na mahojiano marefu iliogundulika kuwa ni uongo na msanii Dulla S aliamua kusema hivyo baada tu ya Choper kukataa kufanya nae kazi kwa kipindi kilichopita na kwa mujibu wa uchunguzi wetu tuligundua ni ugomvi wa kikazi ulotokea kiasi cha miaka miwili hivi iliyopita.
leo tujaribu kutazama maisha ya kimuziki ya msanii Chope ambae amekuwa ni msanii wa kwanza kufanya muziki wa kisengeli kutokea mkoani Arusha.
Chopa alipokutana na 20 percent kwa mara ya kwanza.
Choper alianza kuonekana kufanya vizuri kwa mara ya kwanza akiwa mkoani Arusha na kundi la Machepe ambalo baadae alikuja kutoa nyimbo yake ya kwanza kabisa ambae ilisikika katika masikio ya wana Arusha wengi,wimbo wa kachumbwicho ambao ulikuwa na mtindo wa ajabu ambao uliwashangaza na kuwavutia wengi.
Wengi walionekana kuvutiwa na mtindo huo ambao ulipelekea Choper kupata nafasi ya kuitwa katika majukwaa na baadhi ya wasanii wakubwa nchini Tanzania na kufanya matamasha kadhaa ambayo yaliwagusa wengi wengi kwa kipindi hicho.
Wakati huo,Choper akiwa anatamba na wimbo wake wa Kachubwichu tayari kundi la wasanii wa Jambo Squard nalo lilikuwa likitamba katika mitaa mingi ya jiji la Arusha,na ukilinganisha na muziki alokuwa akiufanya Choper Machepe,kazi ilikuwa kubwa na muziki wa Arusha ulizidi kutambulika sana katika nchi ya Tanzaia
OD wa jambo squard alishiriki wimbo wa CHAPA ILALE.
Mbali na hayo pia,Choper aliwahi kufanya kazi na waandaji wakubwa wa Arusha kama Justino wa Kuka record ambae ndie muandaji wa ile nyimbo maarufu ya kiroba na ile ilotamba katika klabu nyingi,wimbo wa vitoto ulotamba mwaka 2016
Mensen selekta alishiriki vyema katika wimbo wa CHAPA ILALE
Katika wimbo wa chapa ilale ambao una viwango vizuri na ni vigumu kwa mtu wa kawaida kuamini kuwa wimbo huo umefanyiwa ndani ya Arusha tofauti na watu wengi walivyozoea kusikia mtindo wa kisingeli ukitokea Dar es salaam na si mikoa mingine.
Wimbo huo umefanywa katika viwango vya juu na unaweza kuja kuwa tishio kwa wasanii wengine wa Dar es salaam wale wafanyao muziki wa kisingeli.
Post a Comment