Header Ads

test

Washindi wa tunzo za Mabati Cornell wakabidhiwa tunzo zao rasmi katika jiji la Nairobi.


Baada ya kutangazwa washindi wa tunzo za  Mabati Cornel award na hatimae siku ya jana katika jiji la Nairobi ndani ya ukumbi wa Kenya national theatre washindi hao wawili kutoka Tanzania walikabidhiwa zawadi zao walizoshinda katika uandishi wa fasihi na lugha ya kiswahili.
washindi wawili toka nchini Tanzania walitangazwa mwezi uliopitya kuibuka kidedea na kuitangaza vyema nchi ya Tanzania katia utunzi wa mashairi na riwaya.
washindi hao ni ndugu Dotto Rangimoto Chamchua ama maarufu kwa jina la Jini Kinyonga na  mwenzake Ally Hilal.

Ally Hilal (kushoto) Dotto Rangimoto (kulia)


Washindi hao wawili kwa mara nyingine tena wameweza kuitangaza nchio yetu ya Tanzania katika mipaka ya nje ya bara la Afrika na kuonyesha njia kwa watunzi wengine wa sanaa ya fasihi hasa ile ya ushairi  na uandishi wa fasihi.
licha ya juhudi kubwa kufanyika kwa vijana hao katika kuiletea sifa  Tanzania lakini bado vyombo vyetu vya habari vimekuwa nyuma kutangaza tukio hilo la  ushindi mkubwa tofauti sana na vyombo vingine vya habari vya nje ya Tanzania na hata nje ya bara la Afrika.
siyo kwamba nalaumu vyombo vyetu vya habari ila nataka kuvitia mkazo katika kutangaza matukio kama haya yanayofanyika nchini mwetu.
sina hakika sana kama magazeti yetu yaliweza kuandika kwa wingi mkubwa kam yalivyofanya magazeti ya Kenya mfano wa gazeti la Taifa leo ambalo liliandika kwa kiasi kikubwa sana kuhusu tukio hilo.
Ni wakati sasa umefika kwa vyombo vyetu vya habari  kuwaunga mkono vijana wanaofanya juhudi katika kukuza sanaa yao kuliko kuandika habari ziso na msingi kwa taifa.
naahidi kuandika  habari na historia ya maisha ya Dotto na Hilal kwa chache zijazo.

Hakuna maoni