Header Ads

test

Dotto Rangimoto Chamchua aibuka mshindi tunzo ya fasihi na kiswahili ya Mabati Cornel

                                              Dotto Rangimoto  pichani mwenye bahasha
Unapoongelea sanaa ya ushairi katika ukanda wa Afrika ya mashairiki na Tanzania utakuwa unaongelea moja kati ya sanaa zenye changamoto kubwa sana kulingana mwitiko wake ulivyo katika jamii lakini kwa sasa mabadiliko makubwa yameanza kujitokeza baada ya washairi kadhaa wakitanzania wakionekana kufanya juhudi zao kati kazi za fasihi na sanaa yao ya ushairi na kiswahili.
unapozungumzia jina Dotto Rangimoto katika historia ya mpya ya ushairi  wa kitanzania na kimapokeo utakuwa unazungumza mmoja kati ya washairi wa kitanzania walioibuka siku ama miaka ya karibuni na kuonyesha juhudi kubwa zilizopelekea Tanzania kupata sifa mpya katika historia ya ushairi hapa Afrika mara baada ya Dotto Rangimoto kuibuka mshindi katika tunzo za MABATI CORNELL



 Tunzo ya mabati cornell ilianzishwa mwaka 2014 na Dkt Lizzy Attree (Mkurugenzi wa Tuzo ya Caine) na Dkt Mukoma wa Ngugi (Chuo Kikuu cha Cornell, Marekani), kwa lengo la kuthamini uandishi kwa lugha za Kiafrika.
   

tunzo hizo za  mabati cornel zinakusudia kuhimiza sanaa ya tafsiri baina ya lugha za Kiafrika zenyewe kwa zenyewe, na pia kutafsiri maandishi ya lugha nyengine kwa lugha za Kiafrika

Dotto Rangimoto aliibuka mshindi kupitia shairi lake la MWANANGU RUDI NYUMBANI
HILI HAPA:

MWANANGU RUDI NYUMBANI. 
 1. Nimeomba hii simu, mwanangu kukupigiya
, Kuna jambo la muhimu, nataka kukuambiya
 Lahusu Dar Salamu, huko uko jichimbiya.
 Mwanangu rudi nyumbani, Mzizima huiwezi. 

2. Mzizima huiwezi, mwanangu hebu sikiya,
 Panyarodi nao wezi, kilema watakutiya
 Jua hawana mbawazi, watu wanapo'ibiya
 Mwanangu rudi nyumbani, Mzizima huiwezi. 


3. Kila kitu nafahamu, huko yanayotukiya
 Joto kama jahnamu, sababu zenu tabiya
, Si nyingine ni wazimu, wa misitu kuvamiya,
 Mwanangu rudi nyumbani, Mzizima huiwezi.

 4. Mwanangu kukosa kazi, mamiyo ninaumiya
 Kimombo haukiwezi, nao ndiwo watumiya
 Usaili huchomozi, kama bubu wabakiya,
 Mwanangu rudi nyumbani, Mzizima huiwezi.

 5. Foleni mwaita jamu, zimejaa kila njiya,
 Tambuwa yakudhulumu, pia yatia udhiya
 Mlowapa majukumu, huenda wamesinziya
 Mwanangu rudi nyumbani, Mzizima huiwezi.

 6. Upangaji makaazi, kinyaa mwana watiya
 Hasa huko kwa waswazi, pana tabu kuingiya
 Magari kufika kazi, vipi moto 'kitukiya?
 Mwanangu rudi nyumbani, Mzizima huiwezi. 

 7. Tama narudisha simu,mwenyewe asubiriya 
 Rudi sikwepe jukumu, shamba nakuandaliya,
 Ndiyo waanza msimu, na mvuwa za kupandiya
 Mwanangu rudi nyumbani, Mzizima







 
 Dotto katikati mwenye kanzu nyeupe mara baada kutangazwa mshindi tunzo ya meya mwaka 2016/17


 Mbali na Dotto kushiriki katika tunzo hiyo,jumla ya washikiri 140 walishiriki kaitka  nyanja mbalimbali ikiwemo,riwaya,hadithi ya picha,ushairi na kadhalika.
jumla kati ya washiriki wote ni majina machache tu ya washindi sita tu ndio yaliyo tangazwa ambao ni ;
 


Mbaruk Ally - Hali Halisi (ushairi); Hassan Omar Mambosasa - Nsungi (riwaya); Mwenda Mbatiah - Kibweta cha Almasi (riwaya) na Richard Atuti Nyabuya - Umalenga wa Nyanda za Juu (ushairi).


Majaji walikuwa Ken Walibora Waliaula (Mwenyekiti wa Majaji), mwanataaluma na mwandishi; Daulat Abdalla Said, mwanataaluma na mwandishi, anayesomesha Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar; na Ali Attas, mwandishi na mwalimu wa Kiswahili na Kiingereza, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, Japan.



Waziri wa habari, utamaduni na Sanaa Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe amewapongeza wawili hao kwa ushindi huo na kusema ushindi wao "unachagiza juhudi za serikali kuibidhaisha lugha ya Kiswahili."
"Ushindi wa Watanzania hawa ni ushindi wa taifa kwa ujumla," amesema Dkt Mwakyembe kupitia taarifa.




 Washindi wanatarajiwa kupokea zwadi zawadi zao tarehe 13 mwezi ujao
hongera sana Dotto kwa kuitangaza Tanzania kimataifa.

Hakuna maoni