Header Ads

test

MOHAMMEDI YOUSRI;RAIA WA KIMISRI ANAEFUNDISHA KUGHA YA KISWAHILI NCHINI MISRI







Lugha ya kiswahili ni moja kati  ya lugha zinazoendelea kukua kwa kasi na kusambaa duniani huku mataifa mengi yakianza kujikita katika lugha yenye utamu katika mazungumzo.
Lugha ambayo inavutia na kumshawishi mzungumzaji kuitumia mara nyingi kutokana na ladha tamu ya lugha hiyo.
Mohammedi Yousri ni raia wa kimisri aliezaliwa na kukulia nchini misri.
akiwa amezaliwa katika desturi na mila za kuifahamu lugha ya kiharabu lakini kutokana na mapenzi yake yakutaka kufahamu lugha za kimataifa alijikuta akiingia katika uwanja mzito wa kukifunza lugha hii ya kiswahili na hatimae kuifahamu hadi kuja kuwa mwalimu katika chuo kikuu.
Katika harakati zake za kuifahamu lugha hii alijikuta akiamua kutembelea Afrika ya mashairiki ili kukuiza lugha yake
yafuatayo na mahojianio mafupi ambayo niliobahatika kufanya nae akiwa nchini Misri lakini kutokana na mawasiliano nipende kuwaomba radhi kuwa sitoweza kuleta mahojiano yote kwa kuwa hayakumalizika ila panapo majaaliwa nitawaletea nusu ya mahojiano hayo ila naahidi kuwa siku nyingi tutazungumza nae kwa kirefu zaidi iwapo tutapata mawasiliano mazuri.
nilianza kwa kumuuliza.

 MIMI MALENGA - kwanini uliamua kujifunza kiswahili ?

MOHAMEDI-Kuna sababu nyingi, ya kwanza kiswahili ni lugha rahisi na tamu sana wowote akiisoma ataipenda, na ya pili ni lugha ya nchi muhimu barani afrika hasa nchi za afrika mashariki kama t.z na kenya na uganda na ruwanda na burundi, na raia ya nchi hizo ni wema sana na wana tabia nzuri kabisa na niliwapenda niliposafiri t.z , ya tatu ni misri inapaswa kuimarisha zaidi uhusiano wake baina ya nchi hizo na mwanzo wa jambo hilo ni lugha , kwani lugha ni msingi wa kila uhusiano na hii ni wajibu wangu mm mwalimu wa lugha ya kiswahili na asili yangu ni mmsiri kuwaelemisha wanafunzi hapa chuo kikuu umuhimu wa lugha ya kiswahili ili wanafunzi hawa baadaye kushiriki katika maendeleo ya mahusiano ya misri na nchi hizo

MIMI MALENGA -Ulitumia muda kujifunza kiswahili na mpaka kukielewa ?

MOHAMMED- Mm niliaoma kiswahili kwa muda wa miaka minne.. nilielewa kiswahili na nilianza kuandika na kuongea baada ya mwaka mmoja.. ili kiwango changu wakati huu huu kilikuwa chini , nilijitahidi na nilisoma kwa bidii ili kufika katika kiwango unachokiona sana hivi kupitia miaka ya chuo kikuu na nilifiki kiwango cha juu kabisa baada ya safari yangu kule t.z nilisoma sana na niliongea kiswahili sana .. kama unavyojua lugha sio maneno ya kuandika tu bali ni kuongea na mazungumzo na anayeelewa lugha anapaswa kuitumia katika mazungumzo maalumu

 
MIMI MALENGA-Kwa hapa Tanzania wengi bado wanaamini kiswahili siyo lugha ya biashara ama lugha inayolipa kama kingereza,je imani hiyo mnayo watu wa Misri ama mnachukuliaje ama kwa huko Misri kuna fursa ya kibiashara kwa wanaozungumza kiswahili ?

MOHAMEDI-Tazama.. kila lugha ina umuhimu wake, na unaweza kuwa na kitu hujui thamani yake, hali hii ni kama lugha, labda kwangu mm au watu wa misri nafikiri kama mm naongea kiswahili naweza kufanya buashara yangu kule tanzania au nchi yoyote humu afrika mashariki , naongea kiswahili vizuri na ninayo biashara yangu maalumu nitaweza kushinda kule, hii ni kwa mfano, na watanzania au waswahili kwa ujumla wanaweza kufanya kazi hapa misri kama mwalimu wa kiswahili au unaweza kufanya biashara yako hapa ukiwa unajua kiarabu
-
MIMI MALENGA-Uliwahi jaribu kuomba kazi ya kufundisha kiswahili katika nchi za Afrika mashariki ama sehemu nyingine duniani ?

 
MOHAMEDI-Nakwambia mm sasa hivi ni mwalimu wa lugha ya kiswahili katika chuo kikuu maalumu hapa misri, ila natamani kufanya kazi katika nchi yoyote katika afrika mashariki na kuendeleza katika mastar yangu ma masomo ya baada ya chuo kikuu , nikipata fura nitaishika kwa nguvu

MIMI MALENGA-Kwa hapa Tanzania lugha ya kingereza huanza kufundishwa katika shule za sekondari ama upili,na lugha nyingine za kigeni kama kifaransa na kispania hufundishwa katika college,vipi kiswahili katika nchi ya misri huzna kufundisha katika kiwango gani cha shule ?

MOHAMEDI-Hapa shuleni hakuna kufundisha kiswahili.. ila katika kiwango cha vyuo vikuu kuna, kiswahili hufundishwa hapa misri katika viyuo vitatu, cha ain shams , cha alazhar, cha kairo, ni majina ya vyuo kikuu hapa misri.. ila katika shuleni kuna hufundishwa lugha nyingi kama kiingereza na kijerumani na kifaransa na kitaliano na kispania

MIMIMALENGA-Ipi changamoto gani mnazokutana nazo wakati mkendeleza lugha ya kiswahili katika kufundisha kiswahili ?
 
MOHAMEDI-Changamoto.. changamoto, nadhani changamoto pekee sana hivi ni ya vitabu, vipo vitabu ila vitabu vya kisasa vya kufundisha lugha ( kozi ) kama vitabu vya kijerumani na kiingereza, ila viko vingi na nilipata vingi sana nilipokuwa kule Tanzania.
 kwa maoni na ushairi wasiliana nami kwa simu namba +255624010160 au barua pepe ya iddyallyninga@gmail.com

Hakuna maoni