TUNZO ZA USHAIRI TANZANIA
FAHAMU KUHUSU TUNZO ZA USHAIRI TANZANIA
Kuanza kwake na dhumuni la kuanzishwa kwa tunzo hizo.
Taratibu,sheria na kanuni za kumpata mshindi
Nusra M. Haji mshindi wa kwanza wa tunzo ya ushairi Tanzania 2017
Erick Ndumbaro ,mshindi wa pili
Hamisi kisamvu,mshindi wa Tatu.
Tulizoea mara nyingi kuona tunzo tofauti tofauti zikitolewa kama zile za muziki za Kilimanjaro,Kora na nyingine ,lakini washairi wao walionekana kuwa wapo nyuma kidogo katika utlewaji wa tunzo hizo japo kuwa zilianza kiasi cha miaka kadhaa iliyopita lakini zikiwa katika mtikisiko mdogo.
Mwaka wa 2017 utakumbukwa tena katika historia ya sanaa ya ushairi ambako kwa mara nyingine tena tunzo za ushairi Tanzania ziliweza jutolewa na washindi kutangazwa (tazama pichani sura na majina yao)
Tunzo hizi zimeendelea kuleta changamoto na kuwatia moyo washairi wa Tanzania ambao sasa wanaanza kuona thamani ya sanaa wanayoifanya.
Tunzo za ushairi Tanzania zipo chini ya taasisi ijulikanayo kama TANZANIA GATSBY TRUST ambayo ilianza kubuni wazo la kuanzisha tunzo hizi mwaka 2013 na kufikia mwaka 2014 tunzo hizi ka mara ya kwanza zilitolewa.
Wazo la kuanzishwa kwa tunzo za ushairi Tanzani lilitolewa na GERALD BELKIN na kuamua kupendekeza jina la rafiki yake mpendwa EBRAHIM HUSEYN na mpaka sasa tunzo hizo zimepewa jina la Ebrahimu Huseyn .
Tunzo hizini tunzo ambazo hutolewa bila ya ubaguzi wa aina yoyote na kila mtu ambae anakipawa cha utunzi wa mashairi anatuhusiwa kushiriki bila ya kutazama umaarufu wa jina lake kama ilivyokuwa kwa kwa tunzo nyingine.
NINI HUFANYIKA ILI KUMPATA MSHINDI
Upatikanaji wa mshindi wa tunzo hizi huanzia katika hatua kadhaa ili kumpata mshi.
HATUA YA KWANZA,ni kutangaza shindani hili katika mitandao ya kijamii,majarida,vipeperushi,vyomboo vya habari vilivyo rasmi na vile visivyo rasmi ili taarifa kumfikia kila mtu na kwa upana zaidi.
HATUA YA PILI,ni kupokea mashairi yote yaliyotumwa ili kuanza kuyafanyia kazi ya kuingia katika HATUA YA TATU ambayo ni kufuta majina yote ya washairi na kuacha shairi peke yake likiwa linasomeka bila ya kuonekana jina la mtunzi na kuyapa namba peke yake.
HATUA YA NNE,majaji wataanza kupitia shairi moja moja kwa siku,ama wiki kulingana na idadi ya mashairi ambayo yamepokelewa.
HATUA YA TANO,majaji watakutana na kuanza kujadili shairi moja moja kulingana navigezo vilivyowekwa ili kuona ni shairi lipi linafaa zaidi ya mengine au jingine
HATUA YA SITA ni kutoa alama kwa kila shairi kati ya yale yalongaa zaidi ya mengine na hatua ya mwisho yani HATUA YA SABA ni kuhesabu wenye alama nyingi hadi kumpata mmoja ambae atakuwa na alama nyingi zaid ya mwenzake na kisha mshindi kutangazwa
Washundi wa mwaka huu ni ...
1)Nusra Haji
2)Erick Ndumbaro
3)Hamisi kisamvu
Taasisi ya TANZANIA GATSBY TRUST katika kuhakikisha inawendeleza washairi wa Tanzania,imeamua kuanzisha tunzi hizi ambazo zitafanyika kila mwaka huku ikiwa na malwengo ya kuwafanya washairi wa Tanzania kujulikana kimataifa zaidi.
kwa maoni bna ushauri wasiliana nami kwa simu namba +255624010160 ama barua pepe ya iddyallyninga@gmail.com
Mara zote nawapongeza waandaaji, wadhamini, na washiriki wote kwa kufanikisha utoaji wa tuzo hii mwaka jana tarehe 23/09/2017. Pia natoa shukrani za pekee kwa mratibu wa shindano hili na wenzake wote kwa juhudi zao.
JibuFutaHAKIKA Taifa bora halijengwi kwa 'porojo' za midomoni, bali hujengwa kwa maandishi, kanuni, na tunu zilizowekwa kwenye makaratasi ili kizazi hiki na vizazi vijavyo viweze kunufaika.
Kwa kuzingatia hili, tuzo hizi hazina budi kudumu daima na milele.
Wadau na wapenzi wa tuzo hizi, tunasubiri sana kutangazwa kwa tarehe ya mashindano mengine na kitabu kipya cha Mashairi ya Shindano la 3.
Mungu akubariki sana.