IHAIDI AFRIKA
IHAIDI AFRIKA
1)Uliahidi kaka yangu,kulilinda
bara langu
Waumiza moyo wangu,kuiacha nchi
yangu
Uwapi utu wangu,siwaoni ndugu
zangu
Iwapi ahadi yako,kulinda wadogo
zako ?
2)Niliahidi kaka yako,kulilinda
bara letu
Sina nguvu ndugu yako,shida viongozi wetu
Wameficha utu wako,hilo tatizo
letu
Ahadi nakuahidi,kulilinda bara
letu.
3)kaka yangu kila siku,ahadi ni
zilezile
Huku kwetu ni usiku,tena mambo
yale yale
hadi zako za masiku,majuzi na
tangu kale
nimechoka yako ahadi,kulilinda
bara letu
4)Huku kwetu mbona shida,tunayo
demoghasia
Umeshapotea muda,watu wanaangamia
vichenchi vile vya soda,ndivyo wanadanganyia
Kaka yangu sema kweli,kama bara
walipenda
5)Nilitambua mengi sana,ndo maana
nikakimbia
Nilitaka kuungana,muda ulishapotea
Nyumbani tunashidana,na hatuna
mazoea
Hakuna demokrasia,kwao ni
demobandia.
6)kaka yangu nakuita,sikia kilio
changu
Chozi langu lishakata,moyoni
nauchungu
Ni nani wakulifuta,siwaoni ndugu zangu
Ahadi ya bara hili,ni kuzidisha
uchungu.
7)hii ni ahadi yangu,kesho narudi
nyumbani
Kulijenga bara langu,liwe kama la
zamani
Tusiwe tena mafungu,irudi yetu
Amani
Hii ni ahadi yangu,kulilinda bara
langu.
8)ona kaka huku shida,tunavyopigwa mabomu
Wao wanatoa oda,tuchinjwe hata kwa
sumu
Huku wamepaka poda,wenyewe
twajilaumu
Afrika hii ya leo,si kama ile ya
jana
9)hatuna tena upendo,zamani
ulipotea
Tumezidisha magendo,na chuki
twaimezea
Udugu twatupa kando,kiama
twakingojea
Kama mwisho wa dunia,ni hapa utaanzia
10)Kaka timiza ahadi,bara
linateketea
Onyesha yako juhudi,kabla hatuja
potea
Hiyo ndo yetu ahadi,utakayo tulete
Tuaahidi waafrika,Amani
watulindia.
SHAIRI-IHAIDI AFRIKA
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Post a Comment