MWASIFU UPUPU,,-Uledi Bryan
Uledi Bryan,mtunzi wa shairi hili
MWASIFU UPUPU.
Jamani nyie jiweni,kusifu wenu upupu,
Chachu kutia mekoni,yani haitoki supu,
Wangu ni Rambo vitani,hatoshei kwenye kapu,
Ang'aa hadi kukera,ni kama lulu za pwani.
Ni kama lulu za pwani,kifua anacho yeye,
Hao wenu masahani,sio tumdhaniaye,
Tena havuti makini,mwatamani kuwa naye,

Macho ni kama ya paa,madogo tena angavu,
Hata angatupwa jaa,angazidi kuwa mbivu,
Kwangu sihitaji taa,anamulika kijivu,

Ana meno kama kete,na umbo kama ya wema,
Shimo za pua ja Pete,nachosema chanda chema,
Ulimi kama machete,na moyo kama wa mama,
Ang'aa mpaka kukera,ni kama lulu za pwani.
Nitoke kwake kwa nini,ye sumaku Mimi Chuma,
Niwapende wana nini,chuki inawaandama,
Sidondoki kama jani,shina ndani nimezama,

Uled Bryan
Kinda mtunga nudhuma
Kedowa kericho kenya

Post a Comment