Header Ads

test

MAWAZO YANGU-Jerry Lengai

                                                                   Jerry


         MAWAZO YANGU TU
Kuna ukame na njaa, Tangaza unitambue.
Kiki za huyu jamaa, Twataka sera ujue.
Siri ya kua shujaa, Ni jela au ujiue.
Kwa lipi anatufaa?,  Pia ni vema tujue.
Mpe heshima haswaa, Laah! vyeo akuvue.

Hasira ni za ugumu wa maisha ya anasa.
Hadhira ina jukumu la maisha ya siasa.
Wanawaza kuhujumu vibaba vyao kujaza.
Vyakuiba havidumu, hima wana wa siasa.
kidumu chama kidumu, Japo hakizai tasa.

Tazama kwenye mitaa, vijana wamechakaa,
Tumekosa marifaa, Kuthubutu yanofaa.
Vichwa vyetu vyazubaa, Twawaza ngono balaa.
Viongozi ni vichaa, haswaa, 
wanauchungu, walah, hawaendi leba kuzaa.

Malalamiko hayeshii, Na kazi hamzitaki.
Visingizio havishi, Mmekua mafataki.
Ati mvua hinyeshi, Juto likimbia biki,
Vya bure havishibishi, Ni bure hambebeki.
Mnajifanya wabishi, Kumbe kambale samaki.
Ninyi ni viwavijeshi. kwangu siwakaribishi.

Hii nguvu tulonayo, Tusimalize kuzini.
Mihadarati si nyayo, Twendeni kasi kazini.
Shambani soni mazao, Ni soga tu vijiweni.
Uliza hitaji lao, Kuishi ka wa mjini.
Taka kugombana nao, Warudishe kijijini.
Sisi vijana wa Leo. Tutamezaje uzee.

Siasa mpaka vyumbani, kazi hamzitamani.
Kughani kwenu uhuni, Si matani,Na sibuni,
Mnaozani matani, Mwenzenu nipo kazini.
Mkono wenda kinywani, Na wana wenda shuleni.
Kulalama nalaani, Hebu twendeni kazini.
Tuna kipya si kinyemi. Ni kinyimi.
Na kulu mbuzi taakul bil kambau.
©jerrymantz lengai

Hakuna maoni