TETESI-Vicent Uhega aoa kimya kimya
1)Nimsema Kyomushula,Leo ya Fulani zamu
Twampa mke mashala,mke mwenye ufahamu
Na hakika inshaala,nyote unamfahamu
Nakunasihi Uhega,nenda jipatie jiko.
2)Tunakuoza kabinti,kadogo tena karembo
Awe mke wa Visenti,msafiri hadi ng'ambo
Mkasake vijisenti,ila muacha matambo
Nakunasihi Uhega,nenda jipatia jiko.
3)Hivi wasubiri nini,kuoa bhana muhimu
Mke oa mweke ndani,ujue mambo adimu
Ingia bwana ndoani,upate mambo adhwimu
Nakunasihi Uhega,nenda jipatia mke.
4)Usiya hofu maisha,eti yataenda Kombo
Mungu atayanyoosha,yavutie kama wimbo
Mke wako wa maisha,huwezi mchapa fimbo
Nakunasihi Uhega,nenda jipatie jiko.
5)Tunamtaka shemeji,kaka usiweke ngumu
Kuoa siyo kipaji,ndoa inaladha tamu
Ndoa hina mjuaji,ingia utafahamu
Nakunasihi Uhega,nenda jipatie mke.
SHAIRI- UHEGA OA.
MTUNZI-Idd Ninga ,Arusha
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160
TAHADHARI-picha haina mahusiano na Ujumbe wa shairi.
TAHADHARI-picha haina mahusiano na Ujumbe wa shairi.
Post a Comment