Header Ads

test

Matumizi sahihi ya 'AMPASENDI' inayowakilisha "NA" katika lugha,sehemu ya kwanza



Mudhihiri S Njonjolo,muandishi wa makala hii.





MATUMIZI SAHIHI YA AMPASENDI(&),INAYOIWAKILISHA  "NA" KATIKA LUGHA. 

Mwandishi wa Kiingereza Joseph Rudyard Kipling,aliyezaliwa tarehe 30/12/1865 na kufariki tarehe 18/01/1936 kwa kuishi kwake miaka 70 katika dunia hii,hata kuwa katika waandishi waliotumia wakati wao kwa kuandika " Hadithi Fupifupi","Riwaya","ushairi" na "Uandishi wa Habari ",aliwahi kuandika maneno yake ambayo katika lugha ya Kiswahili yanaweza kueleweka kama hivi,

"Maneno ni,kwa hakika ndio katika madawa ya kulevya yenye nguvu zaidi yaliyowahi kutumika na mwanadamu".

Lakini pia,siwezi kuyasahau maneno ya mwandishi wa Kimarekani Nathaniel Hawthorn ambaye ni mzaliwa wa tarehe 04/04/1804 na kufariki tarehe 19/05/1864,ambapo alibahatika kuishi miaka 59 katika uso huu wa ardhi na alipata kuandika kuhusu uzito,nguvu na mamlaka,siri iliyopo katika uwezo wa kuitumia lugha hasa ikitumiwa katika ufasaha wake kwa kusema,

"Maneno-hayana hatia kabisa na hayana nguvu kabisa kama vile yasimamavyo yenyewe katika makamusi.Namna yanavyokuja kuwasilisha uzuri na uovu ni juu ya mikono ya yule tu anayejua namna ya kuyaunganisha(maneno).

Kwa nukuu hizi na zingine nyingi,hunifanya kuzinduka.Na kutamani kuwazindua wengine kwa kidogo ninachokipata katika kupitia pitia kwangu maneno vitabuni, na kila pale yalipoandikwa. Hapana shaka  kabisa  kama mtoto wake kaka  Mateo Mwita,akija kunukuu siku moja kuwa Mudhihiri Saidi Njonjolo mwandishi wa Kiswahili nchini Tanzania alipata kusema,
"Apendaye kuvuna nguvu ya kimamlaka na busara za dunia,basi ajenge urafiki na lugha iliyo fasaha".

Tukiendelea katika somo letu la "Writing Mechanics",leo hii ninapenda kukumbushana katika matumizi ya alama hii ya kiunganishi ambayo nimeyaona matatizo makubwa kwa watumiaji wengi mno,kama ambavyo blogu moja ya Kiingereza inayoitwa "Business Writer's Blog",walivyoliona kwa waandishi wao na kujaribu kutoa ufafanuzi utaowanufaisha ulimwenguni kote. 

Ampasendi(&),kwa kuiwakilisha kwake "na" katika Kiswahili au "and" katika lugha ya Kiingereza au "wa" akatika lugha ya Kiarabu,au "Y" ambayo hutamkwa "iy" katika Kispanyora au “takzhe” katika lugha ya Kirusi nakadhaalika na kadhaalika haifanyi kila inapotakiwa kukaa moja wapo basi na nyengine kuwa na uhalali wa kukaa katika sehemu hiyohiyo. Bali hukaa kwa mpangilio wake na kanuni zake zilizowekwa kama zijavyo hapa chini. 

1.Kwanza kabisa,usije ukaitumia ampasendi(&)katika maandiko ya kubadilika badilika au ya kawaida"regular text",vichwa vya habari au vyeo na vitambulisho badala ya "na" isipokiwa katika mazingira haya tu uletewayo.

i)Majina maalumu kama vile majina ya makampuni.Mfano, "Azam   & Wakita".Hapa unakumbushwa kuiwachia nafasi "space" hiyo ampasendi yako nyuma na mbele isibughudhiwe.

ii)Tumia katika alama"logos",vichwa"titles" na majina ambayo ni alama ya ubunifu au kuundwa.

iii)Tumia katika vichwa vya kazi za ubunifu kama vile riwaya,tamthiliya,shairi,wimbo na albamu au michezo ya filamu n.k.Ampasendi (&)hutumika kuonesha kuwa ushirika mkubwa na wa karibu mno kati ya vile vilivyounganishwa kuliko kutumia neno "na".Umoja wa waandishi wa Amerika " The Writers Guild of America" ambayo ni tofauti na ile ya Uingereza inayoitwa "The Writers Guild of Great British" huitumia ampasendi(&) kuunganisha majina ya waandishi wawili ambao wameandika kazi moja.Mfano,tamthiliya ya "Nje-Ndani" iliyoandikwa na "Majid Mswahili & Mudhihiri Njonjolo" au shairi la "Koja la Bwana Msa" lililotungwa na marafiki wawili "Madaraka Julius Kambarage Nyerere&Mudhihiri Njonjolo",au riwaya ya "Uzalendo" iliyoandikwa na "Wilbert Mahenge&Bimkubwa Abeid" n.k.      

Kwa hakika lugha ikitumiwa vibaya huroga.Wakati lugha ikitumiwa vema hutibu.Kwa dasturi, wachawi hutiya niya kwa kusemezea nyoyoni,halafu waganga nao huja kupindua niya kwa kutia niya njema nyoyoni au hata kwa sauti. Niya ndio zao la lugha. Lugha ina nguvu ya ajaa ukipata alimu au mwenye kipaji cha kuitumia.Kwa andiko hili,liishie hapa na litaendelea tena sehemu yake ya pili ili kukamilisha matumizi sahihi ya alama hii ya ampasendi(&).

Mudhihiri Saidi Njonjolo.
Mtwara-Mjini.
0714-821926.
19,Mei.2018.




Hakuna maoni