Header Ads

test

Vicent Uhega-Mkurugenzi wa taasisi ya sauti ya vijana Tanzania na harakati zake za kuinua ushairi

Amani iwe juu yenu wadau wote na wapenzi wa blog hii mimi malenga.
leo kwa mara ya kwanza kabisa katika kipengele hiki cha mdau wetu tumekutana na mkurugenzi  mkuuw a taasisi ya sauti ya vijana Tanzania (voice of youth Tanzania) Mr Vincent Uhega ambae tumefanikiwa kuifanya nae mazungumzo mafupi kuhusu taasisi yake ambayo  kwa kanda ya kaskazini mwa Tanzania ndio taasisi ya pekee ya vijana iliojikita katika masuala ya kuendeleza vipaji vya vijana ikiwemo sanaa ya ushairi.
Taasisi ya Voice of youth Tanzania ilianzishwa mwaka 2012 mara baada ya kufanyika kwa projrct kubwa ya kusaka vipaji kwa vijana wa mtaani ilijuliana kama TALANTA MTAANI,ndipo baadae baada ya mashaurino marefu Vicent aliamua kuanzisha taasisi itakayo simamia masuala ya vijana wa kitanzania katika nyanja mbalimbali kama elimu ya uajasiriamali,tafiti,michezo,elimu ya uzazi,elimu ya stadi za maisha na sanaa.

                          Vicent Uhega akiwa katika ofisi ya taasisi ya Voyota,iliyopo Usa river.
 Vicent anasema moja katika ya malengo yao makuu ni kuendeleza fani ya ushairi kwa vijana wa kitanzania huku akisema wanamkakati mkubwa wa kufanya mabadiliko makubwa ya ushairi kwa kanda ya kaskazini na Tanzania kwa ujumla.
Alipoulizwa nia mpango gani huo,alijibu ni mapema sana kuzungumzia hilo ila mambo yatakapo kuwa tayari wataweka kila kitu hadharani huku akwaomba washairi wa Tanzania kukaa mkao wa kula kwani mambo wanayoandaa kuyafanya ni makubwa na hayjawahi kuotokea katika ukanda wa Afrika ya mashariki na kati.
Vicent ameendelea kuwahimiza washairi wa kanda ya kaskazini kuendelea kujitoa katika masuala mbalimbali ya ushairi pindi yatangazwapo kufanyika.
Vicent amesema mara kadhaa wamekuwa wakitoa mialiko lakini washairi wamekuwa wakiingia mitini bila ya kuonekana.
Ametolea mfano wa tamasha la Mwananchi Festival ambalo washairi washairi kadhaa walipata mualiko lakini hawakutokea.
Amesema,washairi wamekuwa  ni waoga
kupanda katika majukwaa na wasanii wa muziki kwa kuhofia labda hawatopata mashabiki ama kushangiliwa.
Ameendelea kuwatia moyo kwa kuwaambika kila jambo linawezekana na wao kama taasisi ya vijana wataendelea kuwapoa sapoti washairi pindi watakapo kuwa tayari kushirikia katika matamasha ya vijana kanda ya kaskazini na mkoani Arusha.
Voice of youth Tanzania ina makao yake makuu mkoani katika eneo la Usa river.

Hakuna maoni