UNAMFAHAMU MTEMI NGELEJA WA PILI ?
Sanaa ya ushairi kwa
zama za sasa ni sanaa ambayo licha ya muitikio kuwa mdogo kwa jamii yetu lakini
bado watu wengi wanazidi kujikita katika kuikuza na kuendeza sanaa hiyo kwa
ajili ya kizazi cha sasa na kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
Watu wengi kwa sasa wanazidi kufanya kila njia kwa maendeleo ya sanaa hii
kongwe kabisa dunia.
Mtemi Ngeleja ni jina maarufu katika mitandao ya kijamii hasa kwa
wale ambao wanapenda sana kufuatilia sanaa yua ushairi watakubaliana name.
Ukiingia katika mitrandao ya
washairi Tanzania utakutana na jina hili ambalo limebobea katika utunzi na
umahiri wa mashairihasa yale yakimapokeo.
Mtemi ngeleja ni nani ?
Jina halisi anajulikana kama Baraka Nicholous Ngeleja ama kwa jina maarufu
Mtemi Ngeleja likiwa ni jina analopendelea kujiita ili kujitambulisha katika
jamii ya washairi.
Kila mshairi anakuwa na jina lake
la ushairi na Baraka Ngeleja anapenda kujiita Mtemi Ngeleja kiama sehemu ya kumuenzi
babu yake mzee Ngeleja ambae ni babu mzaa baba.
Mtemi Ngeleja alianza kuandika
mashairi yake mnamo mwaka 2012 akiwa anaandika mashairi katika mfumo wa
mashairi ya huru na miaka miwili baadae yani mwaka 2014 aliamu kubadilika kutoka
katika mfumo wa mashairi ya huru na kuingia katika uandishi wa mashairi ya
kimapokeo au mashairi yale yazingatiayo kanuni na sheria za ushairi.
Mtemi Ngeleja anasema anapenda
sana kuandika mashairi ya kimapokeo kwa sababu yanaleta uimbikaji wake kuwa
mzuri.
Ukitazma mgumo wa mashairi ya
kimapokeo yanakuwa ni rahisi sana kuimbika kkwa sauti zaidi ya moja au zaidi ya
kumi kuendelea na hali hiyo huleta raha kwa msomaji,msikilizaji na hata mtunz.
Mtemi Ngeleja anasema,watu wengi
hupenda kuandika mashairi huru kwa kuwa ni rahisi kwani hayaangalii wala
kuzingatia sheria za ushairi.
Mtemi anawashauri watu wengi kuwekeza
katika ushairi wa kimapokeo kwa sababu
ni aina ya ushairi unaovutia sana na una mamo mengi ndani yake tofauti
na aina nyingine ya ushairi.
Mwaka 2017,Mtemi ngeleja aliamu
kuanzisha kurasa maalumu kwa lengo la kuwakutanasha washairi na wapenzi wa
ushairi duniani,kupena elimu na kusambaza kazi mbalimbali za washairi duniani.
Mtemi Ngeleja ni muaasisi wa page
hiyo maarufu kwa jina la USHAIRI INITIATIVES & POEMS PROJECT au UPP ambayo mpaka sasas
inawanachama toka sehemu mbalimbali duniani,ikiwemo Tanzania,Kenya,Rwanda,Nigeria,GhanaIndia
na sehemu nyingine za duniani ambapo washairi hukutana na kubadilishana kazi
zao.
Anasema,mbali na washairi kukutana
katika UPP pia lengo lake nyingine ni kutaka ushairi upatikane katika mitandao
yote ya kijamii.
Anasema lengo linguine kubwa la
kuanzishwa kwa UPP ni kusaidia washairi kuchapa vitabu na mpaka sasa taratibu
za kutoa kitabu cha mashairi zinaendelea ingawa mwaka wa jana 2017 alifanikiwa
kutoa kitabu kwa lugha ya kingereza kiitwacho
"THE TROPICAL SONGS"
Mtemi Nngeleja anasema mpaka sasa
kupitia kazi yake ya ushairi amefanikiwa kupata marafiki wengi toka pande
mbalimbali za dunia.
Anaendelea kusema kuwa hivi sasa
kazi za ushairi zinapatika kwa wingi hivyo kuwaomba watanzania kuwaunga mkono
kwa kusoma kazi zao ambao zinaelezea maisha yao halisi ya kila siku.
Nilimuuliza,NINI KIFANYIKE ILI KULETA MABADILIKO NA MAENDELEO KATIKA SANAA YA
USHAIRI ?
Haya yalikuwa majibu yake :
WASHAIRI TUNAPASWA KUANDIKA MASHAIRI AMBAYO YANAIGUSA JAMII
BILA KUSABABISHA MGONGANO ULIO WAZI NA TABAKA LOLOTE, LAKINI PIA JAMII
INATAKIWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA WASHAIRI KWA KUNUNUA KAZI ZETU PAMOJA
NABKUTOA USHAURI KIPI TUBORESHE ILI KUFANYA USHAIRI UWE NURU KWA JAMII ZETU.
MWISHO, SIKU ZOTE NASISITIZA SANA UMOJA BAINA YA WASHAIRI, HII ITATUFANYA
TUTAMBUANE NA TUGANYE KAZI KWA NGUVU ZOTE. ASANTE SANA.
Makala hii imeandikwa na Idd Ninga wa Arusha
Tanzania.
+255624010160.
Post a Comment