UNAMFAHAMU MOHAMEDY HOSNY,MTAALAMU KISWAHILI KUTOKA NCHI YA MISRI ?
Lugha ya Kiswahili ni lugha maarufu sana katika ukanda wa
Afrika ya mashariki hasa nchini Tanzania ambako asilimi kubwa ya watu wake
wanakizungumza Kiswahili katika maelewano mazuri licha ya changamoto za kilafudhi zilizopo katika sehemu mbalimbali
ambazo bado pia hazina athari kubwa katika kuporomosha lugha ya Kiswahili.
Si jambo la ajabu leo hii kukutana na watu wengi watokao
mbali na nchi za ukanda wa Afrika mashariki wkijifunza na kuzungumza sana lugha
hii kama vile na wao ni wazaliwa wan chi za Kiswahili.
Hali hiyo inatia hamasa kubwa sana kwa vijana wengi
wazungumzaji na wasio wazungumzaji na wao kujifunza ama kujiendeleza katika
lugha ya Kiswahili.
Mwaka jana niliandika mahojiano mafupi nilofanya na mtaalamu
wa Kiswahili kutoka nchini Misri ambae alikuwa mwanafunzi na baadae kuwa mwalimu
wa lugha ya Kiswahili.
Mohammedi Yousri Mswahili likiwa ndio jina lake maarufu.
Lakini leo tena tarehe moja ya mwezi wa kwanza mwaka
2018,nakuletea makala nyingine ya mtaalamu wa Kiswahili kutokea huko huko
nchini Misri,Mohamed Hosny.
Najua ni wengi sana kati yetu watakuwa hawafahamu kuwa Kiswahili
ni moja kati ya lugha za kitafiti katika nchi ya Misri na wazungumzaji wengi
wakiwa ni wasomi waliobonbea katika masuala ya lugha za kiafrika katika chuo
kikuu cha Misri.
Mohammed Hosny alizaliwa tarehe 29 ya mwezi wa kumi Mwaka
1989 katika nchi ya Misri.
Alizaliwa katika eneo la Al Khanka mkoa wa Al Khalyubiya
Misri ila kwa sasa Hosny anaishi katika mji mkuu wa Cairo.
Pia Mohammed Hosny alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Al Azhar,moja ya vyuo vikuu maarufu duniani vilobeba katika
ufundisha wa masuala mbalimbali yakiwemo yale ya lugha za kimataifa.
Mohamed Hosn anasema,walimu wake wengi wa lugha ya Kiswahili
ni raia ya Misri na pia NI raia wa Tanzania na hata alipokuja Tanzania likutana
na baadhi ya walimu wa Kiswahili ambao walimfundisha na hata marafiki wake
wale wa asili ya kimasai walimfundisha
kuzungumza baadhi ya maneno katika lugha ya kimaasai.
Mohamed Hosny,kulia
Anasema aliipenda sana Tanzania hata kupenda baadhi ya timu
za mpira wa miguu huku timu ambayo anaipenda zaidi ni ile ya Yanga na huku timu
ya Misri aipendayo ni Zameleki ambayo mara kadha tumeshuhudia ikifanya
mashindano na timu za Tanzania kama Simba ya Dar es salaam
Anamkubali sana mchezaji Mbwana Samata ambae alijizolea umaarufu mkubwa
katika bara la Afrika baada ya kupewa tuzo ya mchezaji bora.
Mohammed Hosny ni muhitimu katika chuo kikuu cha AL Azhari
kitivo cha lughana ufasiri kitengo cha lugha za kiafrika akiwa amehitimu mwaka
2014.
Mohammed Hosny kwa sasa ni ni mratibu wa masuala ya vijana katika muasasa ya Nile kwa masomo ya kiafrika na kimkakati.
Mohammed Hosny kwa sasa ni ni mratibu wa masuala ya vijana katika muasasa ya Nile kwa masomo ya kiafrika na kimkakati.
Makala hii imeandikwa na mimi Idd Ninga
Simu namba +255624010160
nitaendelea kuwaletea taarifa mbalimbali zihusuzo Kiswahili panapo
uhai na maajaliwa yake mwenyezi.
Post a Comment