UMUHIMU WA WASHAIRI KUWA WAMOJA
Asalamu alaykum mdau,mshairi na mpenzi wa mashairi Tanzania.
Ni matumaini yangu kuwa sote tu wazima wa afya na mungu mwenyezi katujaalia tena kukutana kwa mara nyingine tena tukiwa na afya na uzima,ashukuriwe sana mwenyezi kwa hilo.
kwa wale ambao kwa namna mmoja ama nyingine wapo katika mitihani basi hatuna budi kuombeana ili wapate wepesi katika mitihani hiyo na sisi mwenyezi mungu atuepushe na mitihani tuliyo nayo.
snaa ya ushairi ni sanaa ambayo bado ina nguvu katika hisia za watu wengi japo kuwa utangazwaji wake wake umekuwa na nafasi finyu katioka jamii.
kengo langu kwa siku ya leo ndugu msomaji wangu siyo kuzungumzia upewaje kipaumbele wa fan hii bali ni kutaka kuanza kuzungumza na wale wenye vioawa na ujuzi wa fani hii ambao wao ndio wenye mamlaka ya kuibeba na kuidumisha taaluma na sanaa hii kwa ajili ya kuifanya idumu na kupendwa zaidi na wana jamii.
najua kulingana na yale nitakayoyaongelea hapa wapo watakao nikubali na wapo watakao kataa ukweli huu ambao nimetamani kuusema na nimeona sasa huu ni muda muaafaka wa kulizungumza ili kwa faida ya sanaa yetu ya ushairi.
UMOJA KWA WASHAIRI ni jambo ambalo sasa ni lazima tulipiganie kwa nguvu zetu zote kuhakikisha washairi wa Tanzania wanakuwa katikia umoja imara na kupendana
ni muda sasa mahusiano ya washairi wengi wengi yamekuwa ni ya kiwango kidogo sana hali ambayo inasababisha washairi wa Tanzania kutokuwa na nguvu katioka kuipigania sanaa yao na hali hiyo hupelekea sanaa hii kuonekana kuwa ni sanaa iliyopitwa na wakati ama ni sanaa ya wazee wa zamani hata kijana leo utakapo simama na kujiita mshairi unaonekana kama mtu ulierudi nyuma miaka mingi na yote hayo ni madhara ya umoja hafifu uliopo kati ya mshairi na mshairi au washairi na washairi wengine.
ukweli usio fichika ni kwamba,kuna washairi kadhaa katika nchi yetu ambao wao kwa kujiona labda kuwa ni wenye ujuzi zaidi ya wengine wamekuwa wakiwadharau washairi wengine na hata wakati mwingine kutokutaka hata kuzisikia tungo za washairi wengine.
Dharau hizo ambazo ni zao la kuwa na umoja dhaifu zimepelekea sanaa yetu ya ushairi kuendelea kubaki nyuma siku zote.
siyo kwamba ushair ihaupendwi,laa.
siyo kwamba ushairi umepitwa na wakati ial washairi wenyewe wamekuwa ni wagonjwa wa kutokupendana,wagonywa wa kutokuwa wamoja.
washairi bado tunamaradhi ya umimi maradha ambayo humfanya kila mshairi kujiona yeye ndie mbora zaidi ya wengine.
lakini cha kujiuliza,swali dogo tu ambalo kila mshairi watanzania na mwenye uchungu na sanaa hii ana weza kujiuliza ni WAKO WAPI WASHAIRI MABINGWA WA FANI HII ?
Jibu la weza kuwa ni lenye kuumiza lakini ni nani leo anae yasikia maumivu hayo hali ya kuwa sisi kama washairi bado kila mtu yupo na njia yake,kila mtu na imani yake,hakuna anaetaka kuwa na sauti moja,kila mmoja ni bingwa mara mia ya mwenzake.
Uwapi umoja washairi Tanzania,kwanini umoja huo hausikiki ?
Kama haupo ni bora kuambiwa kuwa omoja huo haupo na kama upo ni bora kuelezwa unafanya kazi gani kwa ajili ya washairi watanzania.
washairi wa Tanzania umefika muda sasa wa sisi kuwa kitu kimoja,tuungane na tupendane.
bila ya upendo ni nani atatuthamini,ni nani atatuelewa.
sisi ndio walezi wasanaa zote zenye mahusiano na mambo ya ushairi kuanzia muziki na kadhalika,mshairi nai mtu mwenye ufahamu wazaidi ya fani ya muziki lakini kwani muziki uwe juu ya ushairi ?
kuna kosa,tena kosa kubwa,UMOJA,umoja haupo.
mwanzoni hasa wa miaka ya tisini wakati fani ya muziki ilipoanza kushika nguvu hapa nchini,kuliibuka makundi mengi ya muziki,makundi ambayo yalifanya kazi katika mazingira magumu,mazingira ya kukataliwa na jamii walionekana kama vituko katika jamii zao,lakini umoja uliwafanya kuwa na nguvu,nguvu ambayo imewapa heshima hadi leo
kwanini hilo linashindaikana katika wanasanaa wa ushairi ?
ni makundi mangapui ya ushairi yanaanzishwa katika jamii na kuamua kuufanya ushairi katika jamiina kuamua kuipeleka sanaa hii katika jamii.
tukubali tukatae bila ya umoja madhubuti washairi tutaishiwa hewani na tungo nyingi zitaenda na maji.
washairi,ni muda muafaka sasa wasisi kuungana na kushikana ili kuyafikia malengo na kufaidika kama washairi .
Mimi IDD NINGA,+255624010160

safi sana.. wazo zuri na nimeelewa.
JibuFuta