MSIWATUSI WAHENGA.
1)Kama hupendi jinyonge,Ujumbe nakutumia
Ukwingie ukugonge,ukipenda weza lia
Na useme na uchonge,tungo sitoifumbia
Msiwatusi wahenga,kwa zo picha za ajabu.
2)Leo nawapa vidonge,enyi msojitambua
mboronge,ka wanga mnawangia
Kumbe mnaona donge,nyingi hamjafikia
Msiwatusi wahenga,kwa zo picha za ajabu.
3)Pindi mkosapo kazi,wahenga mwawashukia
Wala Hamna ujuzi,kazi yenu kurukia
Mngelikuwa ni mbuzi,chui ningewaitia
Msiwatusi wahenga,kwa zo picha za ajabu.
4)Komeni mkome tena,mfanyacho ukichaa
Na anune wa kununa,hiyo ni mbaya tabia
Mabua utaja vuna,nyani ukimchekea
Msiwatusi wahenga,kwa zo picha za ajabu.
SHAIRI-Msiwatusi wahenga
MTUNZI-Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Post a Comment