Header Ads

test

UZEMBE NA KUTAPELIWA KWA WASANII WA ARUSHA

                 MAKOSA,UZEMBE NA KUTAPELIWA KWA WASANII WA ARUSHA


Mabadiliko makubwa ya sanaa ya filamu na maigizo kwa mkoa wa Arusha yalianza kuonekana wazi kipindi ambacho bwana Chriss Siriwa alipoingiakatika mkoa wa Arusha na kuanza kufundisha sanaa hiyo akiwa na kundi la AGESTA ambalo lilikuwa namasikani yake katikakati ya jiji la Arusha.
Mabadilik,hayo yalipelekea kuzaliwa na kuendelea kukua kwa wasanii na makundi mengi ya filamu na maigizo
Arusha ni moja ya mikoa nchini Tanzania yenye vijana wenye vipaji vingi vikiwemo vya uigizaji,ushairi na kadhalika.
Katika wiki mbili zilizo pita palitokea tukio moja ambalo lilibeba hisoa za wasanii wengi wa mkoa huu ambao bila ya kutegenea walijikuta wakiingia matatani kwa kuitapeliwa bila ya wao kujijua ama kufikiria,au walijikuta wakiwa matatani kulingana na sababu kadhaa ambazo tutaziona mbele
Dhumuni la kuandika makala hii ni kutaka kuwekana sawa ili siku nyingine pasije kutokea tukio kama hilo na kufanya watu kuingizana katika lawama
 Zaidi ya wasanii mia moja wa mkoa wa Arusha walijikuta wakitapeliwa na kupoteza muda wao mwingui huku wengine wakipoteza kiasi cha fedha baada ya kuahidiwa kyushiriki katika project ya picha za video iujlikanayo kwa jina la OLD FASHION AND AFRICAN CULTURE ambayo ilikuwa ifanyike jkatika mji wa Moshi chini ya msanii JOHNSON pamoja na kijana mwingine ambae hadi sasa hivi ajajulikana ni nani kwa sura ila alifahamika pia kwa jina moja la  OMINO
Johnson  ambae ndie muhisika namba moja katika tukio hili baada ya kupata project hiyo aliamua moja kwa moja mkuipeleka katika kampuni ya OSG ENTERTAIMENT ili ashirikiane na vijana na vijana wa kampuni hiyo iliyo chini ya mkurugenzi wake ndugu Isack Chalo lakini kulingana na mambo fulani kutokuwa sawa walijikuta Johnson akivunja mkataba na kampuni hiyo na kuamua kufanya kazi na kampuni na watu wengine ambao ni wasanii wa Arusha badala ya kampuni.

                                 Isack Chalo,mkuruernzi wa kampuni ya OSG ENTERTAIMENT
Ikumbukwe pia kuwa kijana Johnson alikuwa ni mmoja katia ya vijana walokuiwa chini ya kampuni ya OSG lakini aliamu aluomdoka baada ya kuona hatoweza kukamilisha project yake hiyo akiwa na kampuni hiyo na baadae aliamu akumfuata msanii mwingine aitwae Francis lucas ama maarufu kwa jina wangiri   na kumuomba wasaidiane katika kukamilisha zoezi zima la kutafuta watu na wasanii walio tayari kufanya kazi na project ya Johnson N Omino project ambayo ilipelekea watu kuingiza ndani ya sero za kituo kikuu cha polisi mkoani hapa.

                                                               Francis Wangiri pichani
je nini kilichotokea baada ya hapo
je ni nani alokosea
 Wasanii wengi wa mkoa wa Arusha walibeba lawama zao moja kwa moja na kuzipeleka kwa Johnson ambae na yeye alidai kutapeliwa bila ya kujiuliza maswali kadhaa kabla ya kuingia mkataba na Johnson
Wasanii wengi walikimbilia kazi hiyo baada ya kusikia kuwa watalipwa kiasi cha dola sabini kwa siku huku kazi ikifanyika kwa muda wa wiki mbili.
Wasanii wa Arusha hawakutaka kuhoji mapema juu ya kampuni ama watu walokuwa wakifanya nao kazi.
Wasanii wa Arusha hawakutazama mkataba waliopewa kama ulikuwa mkataba kweli ama laa.
Wasanii wa Arusha hawakuhoji ni kwanini kampuni ya bwana Chalo ilivunja mapema makubaliano na Johnson
Wasanii wa Arusha waliamini kupata pesa kwanza bila ya kuuliza pesa hizo zinatoka kwa nani na zitawafikiaje na haki yao ni ipi
wasanii wa Arusha walijikuta wakipigwa cganga la macho baada ya wao kuwa wazembe na kutyokusoma mkataba huu ambao haukuwa na kiwango chochote cha makataba wa mapesa ya zaidi ya shilingi mia moja za kitanzania

                                                           mkataba wenyewe ulikuwa hivi
Kwanza kabisa tutazame makosa yakiyokuwa katika mkataba huo hapo juu ambao hata wasanii hawakutaka kujiuliza wala kutazama makosa hayo
kwanza/mkataba ulionyesha jina la project na haukuonyesha jina la kampuni ambayo wasanii walikuwa wakienda kufanya nao kazi,zaidi wao waliwaza kufanya kazi kwanza ndipo baadae waje kuhoji kampuni hiyi ni i[pi
Na hicho ndicho kilichotokea,wasanii walitaka kujua jina la kampuni baada ya kuwa tayari wameingia mkataba na kugundua kuwa wametapeliwa.
pia mkataba unaonyesha majina ya OMINO na JOHNSON bila ya kuonyesha majina yao kamili,mawasiliano yao,wapi wanakopatikana na kadhalika.
wasanii hawakutazama hili.
pia mkataba hauonyeshi muda wa kuanza na kumalizika kwa kazi hii jambo ambalo hata kesho iwapo Johnson atapekwa mahakamani ataweza kujitetea kuwa muda wa kuanza kwa kazi hiyo haujafika.
Pia wasanii hao walijikuata wakiingia katika mkataba wa mamilioni ya pesa bikla ya kumshirikisha mwanasheria yeyote.
hayo ni baadhi ya makosa walofanya wasanii wa Arusha,makosa ambayo yanapaswa kuwa ni funzo kwa wasanii wengine ili siku nyingine wasijikute wakikimbilia kazi bila ya kufahamu chanzo chake ni nini.
Iwapo wasanii wa Arusha wangekuwa makini haya ya kutapeliana yasingetokea
yapo mengi yalotokea wakati wa mchakato wa kuuandaa project hii,wasanii walifanyiana fitina sana na ni matumaini yangu,baada ya kuandika haya nitakuja kuandika pia kuhusiana na jinsi baadhi ya wasanii walivyowafanyia wenzao fitina ili tu wasije kufanya kazi hii bandia
Imeandikwa na IDD NINGA +255624010160

 

Maoni 1 :

  1. https://mimimalenga.blogspot.com/2017/09/makosauzembe-na-kutapeliwa-kwa-wasanii.html

    JibuFuta